Tuambiane ukweli mbona ni mambo ya kawaida jamani

Jumatatu naamkia makao makuu ya nchi , katika wiki kadhaa nyuma .

Huko nafanya kilicho nipeleka , najipanga kurudi ila nasema wacha nimpigie rafiki yangu mmoja kutoka huko kwa washua ( Wahaya)

Bila ajizi anapokea simu , makutano yanapangwa tunakuwa na muda mzuri sana kwenye kumbi za starehe ila kati kati ya usiku wakati bado tunafurahia mkojo wa sheitwani namuona rafiki hayupo sawa , mwingi wa simu , toka niingie zinakuwa nyingi .

Sasa mimi ni mstaafu najipa muda kutojihusisha na yasiyonihisu , nikiikumbuka kazi ya rafiki yangu kichwani jibu linajipa kuwa basi kuna shida .

Agahalabu sana kumuona katika hali ile , mimi huyoooo na maji yangu naendelea kuburudika nastuka asubuhi nisijue kuna nini nje na wala niliachana na rafiki yangu mda gani , maana hata bye hakuna aliyemtakia mwenzio .

Asubuhi na mapema niko na ratiba nirudi zangi kwa akina Mwaisa niendelee kula mdudu kwa Wagadugu kwa siri sana .

Ratiba inakuwa sawa ili mida ya saa sita niondoke , Mungu yuko nami mimi huyo Green city salama kabisa bila shida , nakaa siku ya kwanza na ya pili mara simu inapigwa kutoka kwa shemeji yangu mkewe na rafiki yangu wa kule mji mkuu .

Ghafla bin vuu ananipa taarifa ya kuumia kwa bwana ake na pia ati yupo Lugalo anaugulia maumivu kaumia kweli kichwani na mguu .

Roho ikaniuma maana jamaa tulispend usiku mzima ila asubuhi no kujuliana hali wala nini mpka napopewa taarifa ya kuumwa kwake .

Haraka sana ratiba inakaa mkao , mama mama la mama anasema kamuone mwenzio , mimi huyo njiani kwenda Dar es salaam kumuona rafiki .

Sasa siunajua tena Lugalo ni mazingira ya kujidai naingia vizuri tu sasa shida namuona mgonjwa ila ameumia kama vile kapigwa na mapanga , mara naona majeraha yaliyo na mashaka utahisi mtu kala chuma .

Nahoji ila majibu hayaniridhishi , basi jioni niko zangu kwenye nyumba ya baba na mama nakula upepeo lakini pia napiga miruzi miruzi kidogo ili hawa wahindi waliopanga hapa wajue mwenye mji niko around leo .


Usishangae napenda wajue ni nyumba zangu na wanipe heshima yangu hata kama nimerithi 😀

Nabahatika kumuona mmoja wao ananipa heshima yangu na kiswahili chake cha kuungaunga nafurahi sasa narudi zangu ndani kuendelea na harakati zangu .

Badae kidogo shemeji yangu anayemkaa dada yangu anapiga simu kunipa hai , anastaajabu mimi kuwepo mjini anaomba tumeet sehemu tupate walau dinner mimi huyo kwa bwana shemeji mpaka maeneo yake ya kujidai.

Kichekesho namkuta yuko chakari sana mpaka nasema bado mimi , ananipa story mbili tatu na mwisho ananipa siri kubwa inayofichwa kwa sasa kuwa baka baka wapo wanakandwa kiaina huko kwenye mji wenye post code 61813 kwa mujibu wa sensa ya 2012

Naamua kukaa kitako anipe full info ndiyo anadai oooh watu wa 925 Kj wapo wanajipanga kwenda kuyaweka sawa ila ukweli wengi washapigika huko .

Duh sina shaka na shemeji yangu maana yupo sehemu ambayo yeye ni mpishi na muandaaji wa taarifa nyeti .

Sasa baada ya taarifa hizo ndiyo napata majibu kumbe jamaa yangu wa mji mkuu siku ile usiku aliponikimbia bar , aliitwa akaitika wito kwa wakubwa zake akazama huko kwenye mji wa post code 61813 ndiyo wakamkunguta na mpaka kuwa vile .

Sasa nikabaki kujiuliza kwanini walinificha kumbe bwana ni oda toka juu watu wasiambiwe kinachotokea huko .

Hapo nikamkumbuka Msukuma aliwatumaga mafia fulani wakawafyeka wale jamaa bila huruma sasa hivi shida nini mpaka rafiki zangi baka baka wanakandwa ?

Afande Mkuu tuelezeni jamani shid ni nini ? Kama wamerudi wale jamaa semeni tu ili sisi wenye ndugu huko tukae chonjo kuwatoa ndugi zetu au tujue kuwa msiba ni muda wowote huko maana wazee wa kazi wapo kazini tena .

Dp world inatosha mimi kuitetea ila huko hata mnilipe mamilioni katu sivai uniform kuingia infront

Tuelezeni tu ukweli ili tujue tunayo haki jamani

Nb
Nimeandika nikiwa nimelewa hata mimi sielewi nimeandika nini .
 
mpeni uprezidar anafaa kabisa
mambo kwangu yamekuwa mengi kwanzia september nitakuwa bize sana
sasa kijiji inahitaji kuwa na president mda wote
watu ninao wapendekeza hapa
muhindi wa kuchoma huyu mda wote yupo.
kondeni anafaa kuongoza maana anabusara
hao wawili wanafaa iliwezakana mmoja apewe uraisi mwingine awe makamo wake,
nitakuwa bize sana maana wageni ndo wanakuja kwa wingi sana sasa tips ndio zitakuwa kipaumbele changu
 
mpeni uprezidar anafaa kabisa
mambo kwangu yamekuwa mengi kwanzia september nitakuwa bize sana
sasa kijiji inahitaji kuwa na president mda wote
watu ninao wapendekeza hapa
muhindi wa kuchoma huyu mda wote yupo.
kondeni anafaa kuongoza maana anabusara
hao wawili wanafaa iliwezakana mmoja apewe uraisi mwingine awe makamo wake,
nitakuwa bize sana maana wageni ndo wanakuja kwa wingi sana sasa tips ndio zitakuwa kipaumbele changu
Duuuh! Hatari sana mimi sifai?
 
Sijui nafeli wapi sijawahi vuwanja bagamoyo mpaka mda huu

dp world wakija hakika kutakuw mji wa kibiashara
 
Biriani za ijumaa na Pilao kabul ni maandalizi tu ya kuja waarabu

Ukijumlisha na Al kasusu unajua hili wazo lilikuw la mda mrefu sana

Wamejenga visima vingi sana kwa misaada mitaani watu wanatumia maji chumvi buree kabisa

Mwezi mtukufu wanatutumia na ngamia za kutosha. Ikifika sikukuu ya Eid huwa najiita Akhmed nifurahie tamu za sikukuuu
 
Biriani za ijumaa na Pilao kabul ni maandalizi tu ya kuja waarabu

Ukijumlisha na Al kasusu unajua hili wazo lilikuw la mda mrefu sana

Wamejenga visima vingi sana kwa misaada mitaani watu wanatumia maji chumvi buree kabisa

Mwezi mtukufu wanatutumia na ngamia za kutosha. Ikifika sikukuu ya Eid huwa najiita Akhmed nifurahie tamu za sikukuuu
Waarabu wanakula Mandi na Zurbian hawali Biryan ni ya wahindi 😂
 
Aisee najulia wapi haya

Ila lile Pilau Kabul la juzi nimelikubali sana
Niombee Dua nipate na mie hela za DP nifungue sehemu nzuri ya kula mandi kama Dubai Biryan kama India yaani cuisine tofauti kama Somali Cuisine Italian Cuisine etc
 
Niombee Dua nipate na mie hela za DP nifungue sehemu nzuri ya kula mandi kama Dubai Biryan kama India yaani cuisine tofauti kama Somali Cuisine Italian Cuisine etc
Unafikiri Watoto wa kidugala akipata teuzi atakuja tena huku kijijini. Kuna uzi wake anadai kijijini wambea sana.
 
Umesoma waratah.wa wakatolik TEC? Hili sakata la dipii wed litatuletea mpasuko mkubwa
 
Hahaha hiii nchi tamu sana
Mtumishi sijui yeye yuko upande gani
Hey wewe kondeni uko wapi kijana ? Leo ni siku ya kanisa kupaza sauti bwana au na wewe ni mmoja wa wana buti la zungu ?😀
 
Kondeni0112 msimamo wako kwenye bandari uko na TEC?
Sijawafatilia hao majasusi pendwa, hapo mpaka kesho, usiku huu ni wakuchati tu na wapendwa, mchana nlikua busy na kazi ya Bwana... ila nko upande wa haki chakula cha watoto ni chakutunza..
 

Similar threads

Wakuu mko gud? Mimi niko gudi kabisa na mshukuru muumba wa mbingu na nchi niko mzima, na nina furaha na amani, nmeshiba, na nina kama afu kumi na tatu za kenyA mfukoni😊 Najua mpaka hapa nitakua nimeshakwaambukiza ka furaha na ka amani kwa wote ambao hamko sawa😀 Kumekuwa na misemo ya hekima...
Replies
9
Views
457
habari zenu.. nimekuwa mtu wa mashaka sana kuingia kwenye maisha ya kuishi na mwanamke,mimi ni mkiristo huwa nafikiriaga sana kubadili dini ilinipate mwanamke aliyeshikilia dini sana,kwa sisi wa kristo huwezi pata mwanamke aliyeshikilia dini haswa,kuna walio okoka ila dini hawajui kwenye...
Replies
18
Views
427
Kwa Nini Levina Alijiua ? Katika toleo la Sauti ya Siti lililochapishwa mwanzoni mwa 1990, mwanahabari Chemi Che-Mponda alielezea kushindwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujibu malalamiko ya mara kwa mara ya Levina ya unyanyasaji wa kijinsia na kifo chake cha kujiua. Shangazi yake Levina na...
Replies
4
Views
251
Kumekuwa na watu wengi wakijitojeza wakodai kuwa kuna madhara kulala na kioo kutazama kitanda. Inaaminika kuwa kulala na kioo kutazama kitanda huleta: Mikosi, Kukosa usingizi, Kuvunjika kwa ndoa, Migogoro, Ndoto mbaya nk., Nadharia hii inatoka wapi? Dhana kwamba hupaswi kulala mbele ya kioo...
Replies
8
Views
454
Back
Top