Ugonjwa wa mabusha sio kwa wanaume tu, hupata pia wanawake.

Hata mwanamke hupatwa na ngiri
Ijumaa, Septemba 22, 2017


Muktasari:​

  • Ngiri maana yake ni kuhama kwa sehemu ya utumbo ama nyamanyama zinazoshikamana na utumbo kutoka katika pango lake na kwenda kujipenyeza na kujihifadhi katika pango la sehemu nyingine mwilini kulikona tishu dhaifu.
  • Wasomaji wengi hunitumia maswali yanayoonyesha kuchanganya kati ya ngiri na busha.

Karibuni wasomaji wa kona hii, leo nizungumzia tatizo la kiafya la ngiri, kitabibu huitwa hernia.

Ngiri maana yake ni kuhama kwa sehemu ya utumbo ama nyamanyama zinazoshikamana na utumbo kutoka katika pango lake na kwenda kujipenyeza na kujihifadhi katika pango la sehemu nyingine mwilini kulikona tishu dhaifu.

Wasomaji wengi hunitumia maswali yanayoonyesha kuchanganya kati ya ngiri na busha.

Busha au kwa kiswahili fasahan ngirimaji, husababishwa na uwapo wa mrundikano wa maji kwenye mfuko wa korodani katika nafasi ya tabaka mbili zinazounda mfuko wa korodani.

Hii hutokana na kuzibwa kwa mfumo wa usafirishaji majimaji kwenye korodani na minyoo midogo ambayo huenezwa na mbu.

Zipo aina mbalimbali za ngiri zinazowapata wanadamu. Ipo ya mfereji wa ndani kwenye nyonga ambayo mara nyingi huwapata wanaume na kitabibu huitwa inguinal hernia.

Huwapata wanaume kutokana na nyama nyama za eneo hilo la mfereji wa nyonga kuwa na udhaifu wakiasili, hivyo kuruhusu tishu za tumboni kujipenyeza.

Aina hii ndiyo huwachanganya watu wakidhani ni busha. Hii ni kutokana na umbile lake baada ya sehemu ya utumbo kujipenyeza katika mfereji wa nyonga unaopitisha vitu vinavyoenda katika korodani.

Aina ya pili ya ngiri ni ile inayojitokeza pia kwenye nyonga, lakini inakuwa ipo nje ya mfereji wa nyonga, ngiri hii hujulikana kitabibu ni femoral hernia.

Aina hii huwapata zaidi wajawazito na wanawake wanene. Tishu za tumboni hujipenyeza kwenye uwazi unaopitisha mshipa mkubwa wa damu unaopeleka kwenye miguu.

Aina ya tatu ya ngiri hujulikana kama ngiri ya kitovu. Nayo hujitokeza eneo la kitovu kutokana na udhaifu wa tishu za kitovuni.

Aina ya nne ni ngiri inayojitokeza baada ya sehemu ya juu ya tishu ya mfuko wa kuhifadhia chakula kwenda kujipenyeza katika uwazi uliopo katika kifua, kitabibu inaitwa hiatus hernia.

Aina nyingine ni ile inayojitokeza baada ya kufanyiwa upasuaji maeneo ya tumboni na hujitokeza baada ya jeraha kupona. Sehemu ya utumbo huweza kuhama katika pango lake na kwenda kujipenyeza kwenye uwazi uliojitengeneza baada ya jeraha kuunga.

Aina hii kitabibu inaitwa Incisional hernia na hujitokeza pia baada ya upasuaji uzazi. Aina hii huwapata zaidi watu wanene na wenye umri mkubwa.

Lakini pia kuna aina nyingine ambazo hutokea kwa uchache mwilini ikiwamo ngiri inayotokea maeneo ya mgongoni.

Takribani vihatarishi vya kupata ngiri huwa ni vile vile, ila sababu kubwa ni kuwapo kwa sababu yoyote ile inayochangia kutokea kwa shinikizo kubwa tumboni na uwapo wa pango ambalo lina tishu dhaifu.

Kuongezeka kwa shinikizo kunachangia kusukuma tishu za tumboni kwenda katika pango jingine ambalo lina tishu dhaifu hivyo kuruhusu upenyaji wa tishu zingine.

Vile vile, uwapo wa dosari au kuzaliwa na maumbile yasiyotimilifu kwa watoto wakiume.

Baada ya kuzaliwa huwa na udhaifu wa tishu za maeneo ya mfereji wa nyonga na kusababisha augue maradhi hayo.

Zipo sababu mbalimbali zingine zinazochangia mtu kupata ngiri, usikose kusoma jarida hili la afya ili ujifunze kwa undani zaidi.


GAZETI LA MWANANCHI
 

Similar threads

Magonjwa Ya Akili Ni magonjwa ya akili yanamfanya mtu kuwa na mtizamo tofauti wa kihisia na kimawazo kufikiria tofauti juu yake Sababu Za Magonjwa Ya Akili: 1. Sababu Za Kibaiolojia Zifuatazo ni sababu za kibaiolojia zinazoweza kusababisha magonjwa ya akili ambazo ni pamoja na; kurithi...
Replies
1
Views
177
Kisonono ni nini? Kisonono ni maambukizi ya bakteria wanaosambazwa kwa njia ya ngono na bakteria anayeitwa Neisseria gonorrhoeae. Hali hii wakati mwingine huitwa 'the clap'. Hii ni hali ya kawaida. Kisonono mara nyingi huambukiza urethra (mrija kati ya kibofu cha mkojo na ngozi) pamoja na shingo...
Replies
2
Views
138
Wakuu kwema? Binafsi yangu kuwaeleza watu kuhusu mipango yangu naona sio sawa maana watu niwajuaji sana wanaweza wakaanza kukushauri negatively au kukukatisha tama...
Replies
13
Views
762
Ukitembea na kuzungumza na vijana wengi wa sasa wanakuambia ukiwa na pesa ‘utang’oa’ demu wa aina yeyote, kwa sababu huwa hawana ujanja panapo mapesa. Na hili linadhihirishwa na wengi wanapobadili wanawake kwa sababu ya uwezo wao wa kifedha. Na hata wanawake wenyewe nao wanaonekana kuhamasika...
Replies
18
Views
383
Katika moja na mbili Jumamosi usiku mwingi sana chimbo flani la walesa mavi, kula vombo kula vombo kula vombo mpaka natambaa, kudadeki wasela mavi wakasepa na kisimu changu cha kutambia mjini pumbavu zao. Nililia kisenge! Silewi tena.
Replies
95
Views
1K

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top