- Jul 8, 2023
- 195
- 704
- 93
Afya n afya ila wote tutakufa .
Hii ni salamu yangu kwenu , mnielewe tafadhali aisee najua kwenye pitapita zako huko mtaani unatamani sana askari ,mara wanajeshi , daktari au hata banker wawe rafiki zako ?
Ni kweli nchi yetu ni nchi ya ulimwengu wa tatu hivyo sikatai umasikini ni mkubwa sana lakini rafiki yangu leo nakupa siri moja ya kuishi na kupanua ubongo wako .
Hao watu sikukatazi kuwa nao karibu ila nakushauri wawe ni jamaa zako tu wasiwe marafiki wa udi na uvumba ? Kwani ushajua nawasema akina nani ? Nawasema wale wote wanaoitwa waajiriwa .
Hawa jamaa hata kama wewe ukiwa mwenzao hawakupeleki popote zaidi mtaishia kukaa na kupeana ofa za pombe , kusindikizana misibani na kwenye masherehe ila jua the great future of your life hawapo nayo kabisa kwanini sasa ?
Ukweli uliowazi ni kuwa waliojariwa wengi ni kuwa wanatoka kwenye familia za chini sana , za kati na wachache familia bora , nakuona unashangaa unasema wewe mzee mbona hatukusomi iko hivi siongelei ajira naongelea viajira yaani walimu , askari polisi , wanajeshi wa vyeo vya kati na chini , watendaji , manesi , madaktari ila wengi wasio maMD nawasema hawa wa siku hizi eti Clinical officer .
Hawa ndiyo ninakuomba wawe jamaa zako ila usiwavute kuwa marafiki , nakuona unajiuliza hawa wanatoka local families ndiyo maana nisiwe rafiko nao , hapana rafiki nielewe umasikini ni tabia na ni utamaduni , nikuweke wazi kuwa kama unaye rafiki mtaani kwenu mnaemwita wa kishua , mtizame kama ana tabia za umbea umbea , unafiki , kufuatiliana , kujiona , ni wachache sana ila sasa mkute mtoto wa mama Asha wa keko juu
Ndiyo utajua nini maana ya kulinga na kujiona kisa ana kiakiba cha elfu nne mfukoni
Sasa turudi kwenye mada mbali na changamoto iliyojitokeza miaka ya karibuni ya ajira ila itoshe kukuambia ukweli kuwa hizo kada tajwa hapo juu hapo miaka ya nyuma kidogo ilikuwa ni ngumu kumkuta mtoto wa familia bora kwenye hizo kazi , ukweli mchungu ila nivumilie sijalewa niko sawa tu .
Sasa ni kuwa kwakuwa hizi kada mara nyingi waliojazana ni watoto wa kambalee basi uhama na tabia zao toka makwao yaani unafiki , wivu uliokithiri , majungu na kufuatiliana ndiyo maana jamii ya watu hawa wao maendeleo yao ni kuwa na kigari namba E , kanyumba ka vyumba vitano na tumifugo twa kuku , hapo anajiona ametoboa humwambii kiti
Japo ukweli mchungu ni kuwa vyote wanavipata kupitia mikopo inayowaumiza mpka wanastaafu hivyo rafiki yangu mwanakijiji watu wa namna hii wewe unayewaza kuwa billionaire mara millionaire hawawezi kukupa mawazo chanya yoyote zaidi watakuonesha fursa ambazo tayari zishawahiwa .
Ndiyo wao ni mabingwa wa kuiga fursa zilizokwisha fanyika , leo atakuambia watu wa bajaji wabapiga hela , naye atakopa anunue bajaji siku mbili anaomba pooh mara madereva ni shida .
Mara matikitiki yana hela naye atakopa aweke hela huko , mara hela za kudownload .
Mwanakijiji hapa naziongelea hizi kada tajwa hapo juu hawa hawawezi kuona mbali ila karibu nako kwa kugeza mambo ya wengine .
Sasa mimi nakushauri jenga sana urafiki na mtu yeyote aliyejiajiri hawa ndiyo mataikon wenye hela na wenye kujua wapi hela iwekwe na kipi kitatokea , nisikilize wewe mwajiliwa uliwahi kujiuliza kama usingeajiriwa je ungefanya nini ?
Nakuona unatoa macho tu , ila hilo swali ukimuuliza aliyejiajiri atakuambia nilitaka kuwa daktari ila mimi sasa ni mjasiriamali na pia bado anaishi vizuri vipi wewe ?
Basi ukweli ni kuwa waheshimu sana watu waliojiajiri , kaa nao karibu wana siri nyingi ambazo hawawezi kukufungukia mpaka umewaweka karibu ila jua wana hela .
Ni watu wenye vingi visivyoonekana ila vinajitambulisha , wewe mhitimu , wewe muajiliwa na wewe mtafuta ajira kaa karibu na watu wa kujiajiri wanazo funguo zako za mafanikio .
Ndimi mzee mwanakijiji.