Young Africans Special Thread

KijijiForums

Official Account
KF Moderator
Joined
Jun 5, 2023
Messages
26
Reaction score
57
Points
0
Historia ya Klabu ya Yanga SC inatokea tangu enzi za miaka ya 1910, ingawaje historia kamili ilianza kuandikwa mwaka 1935.

Kulikuwa kuna timu inaitwa New Youngs ambayo Mwaka 1935 uwezo wake ulishuka sana kusababisha wanachama kutofautiana na kuleta migogoro katika Klabu na ukasababisha baadhi ya wanachama kujiengua na kuanzisha Klabu nyingine baada ya New Young’s kushuka Daraja.

Wanachama walioondoka waliunda Klabu iliyojulikana kwa jina la Queens FC. ambayoa baadaye ilibadilisha jina na kuitwa Sunderland ambayo kwa sasa inajuliakana kama Simba SC.

Kabla ya kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs vijana wa Dar es Salaam walikuwa na desturi ya kukutana viwanja wa Jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani Boys
Ndani ya kipindi kifupi timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo, miongoni mwao waliovutiwa na uanachama wa klabu hiyo ni Tabu Mangala (Sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926 walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi sasa kuna shule ya sekondari ya Tambaza.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo bandarini.

Baada ya mkutano huo, timu ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika.

Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana wa Jangwani hao.

Enzi hizo kikosi cha Yanga cha ushindani kikiwa uwanjani tayari kwa mchezo

Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wanatembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani wao, kwamba katika kipindi hicho wao ndiyo zaidi, kwa sababu Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Italiana.

Taliana FC ilipata mafanikio ya halaka na haikushangaza ilipopanda ligi Daraja la pili kanda ya Dar es Salaam.

Mwanzoni mwa miaka ya 1930 Taliana waliamua kuachana nalo mapema kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs.

Kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu vipya pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs waliweza kutwaa kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.

Hatimaye ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs 1935 wakati baadhi ya wachezaji walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland kutokana na New Youngs kushuka Daraja.
 
no offense, ila mzee nikiangalia replies zako, na iyo avatar hapo, huwa sijui nawaza nini 🥹
avatar umeitoa wapi mzee 😃
Hiyo avatar ni kutoka kwa animation ya Moana. Ngoja nikuwekee link undone

To view this content we will need your consent to set third party cookies.
For more detailed information, see our cookies page.
 
Mimi sijui vizuri mambo ya mpira. Ila nimejitoa kwaajili ya huu uzi wa yanga, umepoa saana
 
wananchi leo tuna jambo letu,haya tuanze kusogea taratibu kwa kideo kushuhudia maajabu
 

Similar threads

Post pictures of men in dangerous situation. Must complete task.
Replies
45
Views
604
Have you never read this novel? Okay get in touch and discuss here
Replies
0
Views
326
Shalom wakuu Pamoja na kua serious na maisha mwili unahitaji ku refresh na refreshments moja wapo ni kucheza games. Hua nahakikisha PC yangu haikosi magemu haya japo ni ya zamani 1. GTA vice city 2.gta San Andreas 3.project IGI cover strike 4.project igi i am going in (the mark) 5.delta force...
Replies
7
Views
722
Je una maujanja yoyote kuhusu kamari za casino? Weka hapa Ndo mahala pake Kuna muda tunahitaji hupunguza stress baada ya mihangaiko ikiwemo kwenda casino. Nikizungumzia casino Kuna mambo mengi sana, bitches kamari pombe anasa na ushetani wa Kila aina Hapo kwenye kamari ndo NAkazia zaidi kwani...
Replies
13
Views
729
  • Sticky
FC Barcelona Even before they changed the football landscape by inventing the tiki-taka style of play, FC Barcelona have been known for their likable and highly watchable brand of football that always seemed to produce results. During their long and immensely successful history, they have won...
Replies
10
Views
296

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top