Aina za Mbu na tabia zao 🦟🦟🦟

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Anonymous

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
515
Reaction score
143
Points
0
Mbu kiswaswadu


Huyu ni mbu msumbufu sana mara nyingi huwa hawahangaiki saaaana na damu ila wao ni kukukera tuu,yaani anakuja kama amekosea njia hivi atakupiga kumbo huku sikioni au puani alafu yeye huyooo anatimka anakuacha wewe unajimamanyua bonge la kofi kama zoba vile. Aina hii ya hawa mbua mara nyingi wanapatikana mkesha wa msibani.





Mbu changudoa


Yaani huyu mchana kweupe hata kama jua linawaka vipi yeye yupo na atakuja atalamba damu na kusepa.huyu mara nyingi anapatikana mashambani au sehemu yenye utulivu na muonekano wake ni mweupe mistari na weusi (kama pundamilia) na ni msafi balaa.





Mbu liwalo na liwe


Huyu ni wa rangi ya kaki yaani yeye hata uwe mkali vipi atakunywa damu tuu labda umuue na ni mbishi ukimfukuza anatoka hapo anahamia pembeni kidogo yaani hatimki hadi anywe damu. Na huyu pale alipokuuma panawasha sana na kuota li lenge lenge la maji.hawa mara nyingi wako kila sehemu sio mchana sio usiku.





Mbu utajua hujui


Huyu akija yeye ni kimya kimya anapiga pafu moja la maana ule mda wewe umeshtuka yeye kashajaza tank nduki unabaki unajilaumu tuu.





Mbu seng*


Yaani huyu kazi yake ni kukukera tuu yaani hatui kwenye mwili wako ila akipita karibu na wewe anatoa mlio mkali kama (miling mashine)au crosing mashine)ile mashine ya kuchonga vyuma. Hawa utasikia mlio wao tuu ila kila ukitaka hata kumwona humwoni unaambulia mlio tu
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
haha hawa mbu ni ndugu zako maana unawajua vizuri sana😀
 

Similar threads

Mlo wako sio tu kile unachokula. Pia ni kile unachosikiliza, kutazama, kusoma, na, muhimu zaidi, watu unaoshiriki nao. Chakula huathiri afya yako ya kimwili, lakini mambo haya mengine huathiri afya yako ya akili na kiroho. Huwezi kula vizuri, kisha ukatazama na usikilize vitu ambavyo...
Replies
7
Views
968
Umwa sana Hitaji pesa Anzisha biashara/shughuli yenye kuwahitaji sana Oya wakuu hii ni quote tu marafiki wapo na wanafiki wapo watakupenda kwa namna flani ila baada ya muda hawako na wewe Tupambane together tuijenge KF as members
Replies
11
Views
312
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya watu milioni moja duniani kote wanaambukizwa magonjwa ya zinaa kila siku. Magonjwa kutosikia matibabu ni tatizo kubwa la magonjwa ya zinaa (STDs) au (maambukizi ya zinaa) na ni kikwazo kikubwa katika kudhibiti magonjwa ya zinaa, WHO ilisema...
Replies
10
Views
254
Habari Wanakijiji... Natoa fursa kwa mabinti warembo watatu(3) wenye uzoefu wa utengenezaji wa fresh juice aina zote kwa kiwango cha juu na wanaozingatia usafi sana. Eneo ni Bar maarufu iliyopo Dar Es Salaam, maeneo ya Tabata inafahamika kwa jina BARACUDA BAR & LOUNGE. Malipo ya kazi nalipa...
Replies
73
Views
918
Kiblia majina yamebeba tabia na mamla na wakati mwingine roho, kila jina linakua na maana yake. Na ukipewa jina baya uwezo wa wewe kuwa na tabia mbaya ni mkubwa sana. Mathayo 18:20 Kwa kuwa wanapokusanyika pamoja watu wawili au watatu kwa Jina langu, mimi niko papo hapo pamoja nao. Jina la...
Replies
31
Views
747

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom