KITU PEKEE AMBACHO MTOTO ANAHITAJI KUTOKA KWA BABA YAKE

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Urban Edmund

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 26, 2023
Messages
636
Reaction score
1,321
Points
0
KITU NACHOTAKA BABA NINAHITAJI KUSOMA
Hodi hodi naingia, baba bora umekuja
kuna jambo kukwambia, nisikize mara moja
shairi nakusomea, sikiliza zangu hoja
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

wala 'sinipe kibaba, na shamba la kulima
eti unipe mbaba, na ndoa ya mapema
so niishie la saba, itanikuta nakama
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

sitaki watu kukaba, wala kwa watu kulima
eti mbeba kiroba, na kuwa mtu wa njama
sitaki kuwa kahaba, niwe wa nyumbani mama
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

sihitaji lako shamba, na mbuzi wako bandani
wala usinipe mavumba, sivitaki asilani
ukitaka mi kutamba, nipeleke tu shuleni
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

elimu kiniachia, kamwe haitaondoka
pesa zitaniishia, naweza kufirisika
mbuzi wataniibia, mashamba yatauzika
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

baba yangu mi mwanao, naomba nisikilize
sitaki yako makao, na tena usipuuze
shika nisemayo leo, kwenye kichwa uyatunze
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

niache tu napambana, baba nipe mahitaji
utafanya cha maana, utakuwa mwekezaji
vilabuni utajivuna, hawatakunywa maji
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

niweze jitegemea, nifanikiwe chuoni
utapata manufaa, utajua tu mbeleni
ufukara kuzuia, kuondoa maishani
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

kama kweli wanipenda, elimu weka ya kwanza
iwe moshi na mpanda, na usukumani mwanza
popote nitakapoenda, elimu itanitunza
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

baba leo ukienda, kwa Mungu kitangulia
malengo niliyounda, nani tanitimizia
sio nasema napenda, hebu jaribu fikiria
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

basi niachie mali, mbayo haiathiriwi
mali hiyo ni daftari, mali hiyo hailiwi
hii ni kubwa siri, wengi wao hawajuwi
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

leo hapa naishia, siwezi kuendelea
ukweli nimekuambia, ujumbe mekufikia
baba nakutegemea, elimu yangu simamia
kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma

Fanya ufanyavyo usiruhusu ujinga utawale ndani ya nyumba yako somesha watoto wako
 

Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
KF Moderator
Joined
Jun 4, 2023
Messages
7,609
Reaction score
26,404
Points
113
Ni sahihi kabisa na nimeupenda huu uzi sana kulingana na mada za kipuuzi zinazowekwa jukwaani

Ni hivi urithi ambao unaweza mpatia mwanao ni ELIMU. Hakuna urithi mwingine unaoweza mfaa mtoto kwa sababu mali huuzwa lakini elimu na ujuzi ni vya kwako. .
 

Urban Edmund

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 26, 2023
Messages
636
Reaction score
1,321
Points
0
Ni sahihi kabisa na nimeupenda huu uzi sana kulingana na mada za kipuuzi zinazowekwa jukwaani

Ni hivi urithi ambao unaweza mpatia mwanao ni ELIMU. Hakuna urithi mwingine unaoweza mfaa mtoto kwa sababu mali huuzwa lakini elimu na ujuzi ni vya kwako. .
natamani sana mwanangu Asome coz hata watoto wa Dangote wamesomeshwa
 

Similar threads

Ushalala kwa mwanamke? Ulikuaje? Ulilala kwa amani au ulikua uahofia njemba atakuja kugonga hodi saa yoyote? Wadau wanadai hatakama unalipa kodi kulala kwa mwanamke ni mwiko maana kuna alie lipia umeme, mwingine gas, na kuna alie nunua saboofer
Replies
0
Views
269
Nawasalimu, alafu moja kwa moja kwenye mada. Mungu amekuwa akikuonyesha kibali kila siku, je, unashukuru vya kutosha kwa kuona hivyo? Je, unaweza kuona hata ishara ndogo kabisa ya uaminifu Wake katika maisha yako? Siri ya kuwa na maisha utele ni kushukuru...... Yesu alipoinua ile mikate 5...
Replies
6
Views
402
Ukitembea na kuzungumza na vijana wengi wa sasa wanakuambia ukiwa na pesa ‘utang’oa’ demu wa aina yeyote, kwa sababu huwa hawana ujanja panapo mapesa. Na hili linadhihirishwa na wengi wanapobadili wanawake kwa sababu ya uwezo wao wa kifedha. Na hata wanawake wenyewe nao wanaonekana kuhamasika...
Replies
18
Views
383
kitu gani umekaa nacho mda mrefu kuliko kawaida, kiatu, nguo, simu, saa, notebook, mkanda, meza, shuka, mto, cheni, miwani, radio, kata kucha,... mimi kuna mkanda nmeuvaa kwanzia form one mpaka leo upo nimeuona leo nmeusikitikia sana...
Replies
23
Views
514
Hi Mimi napenda romance sana sana na zaidi tuwekane love beat kabisa icho ndicho napenda
Replies
93
Views
3K

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom