Kwanini MAUTI huogopwa..

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

The great manenge

New member
Platinum Villager
Joined
Jul 8, 2023
Messages
1,320
Reaction score
2,995
Points
0
Daaah hii mada ngumu kumeza haina haja ya salamu...

Kichwa chenyewe kokii.
Lazima kikufikirishe pia kikupe uoga tuu.

Tunaanza hiviii.

Kifo ni ile hali ya uhai kutoka ndani ya kiumbe hai chochote. Kifo kinaweza kumtokea mtu, mnyama, bakteria, kirusi, mmea, jani n.k. Vyote hivi maadamu vina uhai ndani yao, vinapotokwa tu huo uhai basi vinakuwa vimekufa.

Lakini Mauti ni nini?

Mauti ni kile kile kifo, isipokuwa ni mahususi tu kwa mwanadamu.. Huwezi kusema “mti” umekumbwa na mauti, au “mbwa” amepatwa na mauti.. Bali utasema, mti umekufa au mbwa amekufa. Ni mwanadamu tu ndiye anayekumbwa na mauti
Lakini kwanini Kifo kitofautishwe na mauti?

Ni kuonyesha uzito wa hali hiyo kwa mwanadamu.. Kwamfano “Kilio” kinaweza kutokea kwa mtu yeyote yule, iwe ni mtoto au mtu mzima Lakini kikiwa kwa mtu mzima, hakiwezi kuchukuliwa kama kile cha mtoto, kwasababu kama vile wasemavyo wanajamii, “ukiona mtu mzima analia basi ujue kuna jambo”

Maana yake ni kuwa hadi mtu mzima anatoa machozi, ujue hayajaja bure bure tu, bali yana sababu nyuma yake, na matokeo mbele yake, kwasababu si desturi ya mtu mzima kulia. Nyuma yake utagundua aidha kuna msiba, au magonjwa, au kuumizwa moyo kusikoelezeka, kusalitiwa au kupoteza mali zake nyingi, au vitu, n.k.. Lakini mtoto mdogo anaweza akalia kwasababu zisizokuwa na maana au msingi wowote.

Vivyo hivyo katika kifo na mauti ni tendo lilelile..kuondoka kwa uhai.. isipokuwa linapokuja kwa mtu, linakuwa na uzito wa namna yake, kwasababu mwanadamu hakuumbiwa kifo, halidhalika kwa sifa yake na heshima na akili alizopewa na Mungu, jambo kama hilo ni anguko kubwa sana kwake..Mauti ni pigo kwa mwanadamu.

***Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”



Japo kifo kinauma sana lakini kinaleta usawa fulani hivi.
Japo kifo kwa upande wa dini ni kama adhabu , lakini I'm sure kwa aina ya maisha na wanadamu tulivyo sasa hivi na ubinafsi huu kama kusingekuwa na kifo maisha yangekuwa mabaya sana.

Nyoka akamwambia mwanamke, “Hamtakufa!" (Mwanzo 3:3,4). Na hili ndilo fundisho la umizimu linaloendelea hadi sasa ya kwamba mtu akifa anaenda kuishi mbinguni kama akitenda mema na anaenda kuchomwa moto akiwa kuzimu (zingatia muda anachomwa moto yupo hai) au Purgatory anapotakaswa dhambi., haya ni baadhi ya mafundisho ya umizimu na uongo ambayo alianzisha shetani edeni!

Je mtu akifa anaenda wapi!? Biblia haikukaa kimya! "Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa." (Mhubiri 12:7). Wengi wamekuwa wakijiuliuza roho ni nini, je ndicho kinawafanya watu waone wakifa wanaenda mbinguni! Ayubu ameeleza juu ya roho. Ayubu 27:3 (Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu,Na roho ya Mungu i katika pua yangu;). Unaweza kujuliza roho inakaa kwenye pua? Jibu ni kuwa roho ni pumzi. Kwa kiingereza muhubiri 12:7 inasomeka "and the dust returns to the earth as it was, and the life's breath returns to God who gave it." Eccl 12:7.
Hivyo mtu akifa haendi popote kwani mwili unarudi mavumbini na pumzi humrudia Mungu kumbuka Mungu alipomuumba mwanadamu alimpulizia pumzi ili awe kiumbe hai. Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai". Hivyo kifo ni Pumzi-Mavumbi = Kifo. Hivyo fundisho la Mungu linabaki kuwa mtu anakufa kwa hakika!
Je hali ya mtu aliyekufa ipoje?
(Muhubiri 9:5) kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.Hivyo mtu akifa hajui lolote. Ni sawa na mtu aliyelala hajui kitu kinachoendelea duniani, ni sawa na mtoto ambaye hajazaliwa wala hajui kama atazaliwa wala hajui kama kuna dunia na mambo hake yanayoendelea.
Muhubiri 9:10 Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe." Hakuna linaloendelea huko kwa wafu, wala hawajui lolite linaloendelea si dunia wala mbinguni!
Hivyo ndugu usidanganywe kuwa waliokufa wanaenda kuishi sehemu kwani biblia imeweka wazi kuwa wafu hawajui lolote. Iweje wewe uamini kuwa wafu wapo mbinguni au motoni, Mungu alikwisha sema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa,. Hebu tambua hili leo ubadilishe mtazamo.
 

Similar threads

Wakuu kuuliza sio ujinga Hivi haya matairi yaliyo nyanyuliwa inakuwaga ni kwasababu gani maana nmejaribu kujiuliza Je niili yasichafuke? Au yanapancha? Au gari alina mzigo? Au linapunguza ulaji wamafuta? Au linatumika kama breki😄 Wadau mnisaidie, au yamechoka yanpokezana na wenzake kwa zamu?
Replies
7
Views
88
Niaje wakuu, hivi wabongo wanawazaga nini? Unakuta mtu anawazazi kijijini wakati wazazi wako hai hawajengei nyumba na hela ipo.. Ila mzazi akifa tu ndio anaanza kujenga kwa fujo(wiki moja), hizi hela za kujenga nyumba haraka hvi zinakuwaga wapi sku zote?.. Unajiuliza inamaana marehemu hakustaili...
Replies
7
Views
127
Nina maana ukipata watu 20 au 30 kila siku mtu mmoja anatoa 5000 au 10000 na kila siku mtu mmoja anatoka. Siitatusaidia kidogo kupambana na maisha. Wewe ni prezidaa uwezi kimbia ukaacha app
Replies
102
Views
2K
Mniwie radhi sina mpangilio naandika kadri vinavyokuja kichwani.... 1. uovu wa bure (uovu usio na lengo) Inajulikana kwamba yote yanayotokea hapa duniani, mazuri kwa mabaya, yamepangwa na Mungu.... yanatokea kwa sababu. Lakini kuna mambo mengi mabaya yasiofafanulika yanayotokea kwa watu wasio...
Replies
40
Views
654
Samaleko... Binafsi natumia Dolby perfume na Amara deodorant kwa sababu zinanukia vizuri na pia ni very affordable kwa majobless kama mimi. Wewe unatumia ipi? Share with us!
Replies
36
Views
700

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom