mshamba_mkuu
New member
- Jun 4, 2023
- 1,563
- 4,525
- 0
Mniwie radhi sina mpangilio naandika kadri vinavyokuja kichwani....
1. uovu wa bure (uovu usio na lengo)
Inajulikana kwamba yote yanayotokea hapa duniani, mazuri kwa mabaya, yamepangwa na Mungu.... yanatokea kwa sababu. Lakini kuna mambo mengi mabaya yasiofafanulika yanayotokea kwa watu wasio na hatia kabisa.... mfano, matetemeko ya ardhi, mafuriko.... yanauwa watu wengi ikiwemo watoto wadogo kabisa wasio na hatia. Nini hasa lengo la haya kutokea?? Mungu mwenye upendo analeta watu duniani ili wateseke??
2. Miungu inafanana na tamaduni zinazowaabudu
Kwakua Mungu ndie muumba wa ulimwengu basi anapaswa asiwe na ubaguzi wowote ule, ajulikane na viumbe wake wote. Kwa sasa kuna dini zaidi ya 4000 duniani.... kila dini na mungu/miungu yake. Kila dini inaamini mungu/miungu yake ndo imeumba ulimwengu. Lakini angalia.... tuchukulie mfano dini ya kikristo na mungu wake, Yahweh. Hii dini inaamini kwamba Yahweh ndiye muumba wa watu wote, lakini hata ukisoma vitabu vyake, matukio yote yanatokea kwenye sehemu za uarabuni na mediterranean, ambapo dini hii imezaliwa. Kwanini huyu Yahweh hakuhusiana na watu wa asia, africa na pengineko??
Miungu inafanana na tamaduni zilizowatengeza, 'gods are a reflection of the cultures that created them' watu wakiushaunganika na kuunda jamii, watakua na maswali 'tumetoka wapi??' 'jua linawakaje??' 'mtu akifa anaenda wapi??' kwahiyo wanatengeneza miungu na kuipa nguvu kwenye fikra zao, ya kujibu haya maswali, na pia kutengeneza mifumo ya sheria za kuongoza watu. Angalia jinsi ambavyo dini nyingi zinakaa kwenye upande wa kukandamiza wanawake. Ni kwasababu tamaduni za zamani zilikua hivyo, na miungu ikatengenezwa kuendana na hali hiyo, miungu ilitumika kama mfumo wa sheria....
3. Mbinguni na Kuzimu
Karibia dini zote zina sehemu mbili ambapo mtu anaenda baada ya kufa kulingana na matendo yake. Kuna mbinguni, sehemu wanayoenda wenye mazuri, na kuzimu, sehemu wanyoenda wenye mabaya. Na sehemu hizi ukienda ndo unabaki huko milele... Sasa tunatambua kwamba ili chochote kiwe na thamani, lazima kiwe na mwisho.... Maisha ni mazuri kwasababu yana mwisho.... Sasa iweje kuishi milele huku ukiungua, ama kusifu na kuabudu... hufanyi chochote kingine, ikawa ni kitu kizuri?? Jaribu kutafakari.... Labda kama unafanya hivyo, usiwe na akili uliyo nayo sasa yaani mungu akuondolee uwezo wako wa kuamua(free will)
4. Hofu ya Mungu
Tunajua kabisa kwamba mungu ndie muumba wa vyote, na mwenye mamlaka.... sasa kwanini atake kuogopwa na viumbe wake?? Kwanini?? Nguvu zote anazo yeye, lakini bado anataka umuogope, itamsaidia nini?? umsujudu na kumsifu, itamsaidia nini?? mtasema sababu zake hazijulikani lakini kwanini atawale kwa hofu, kwanini anahangaika sana na sisi viumbe wa chini?? Ukinywa pombe, ukizini, anakasirika.... kwanini?? ina maana anapata furaha kupitia hofu yetu.... je, ni kitu kizuri hiki?? anakupa uhuru wa kuamua, ila kuna vitu ukiamua anakasirika, huu ndo uhuru?? Jiulizeni maswali haya....
5. Kwanini hajidhihirishi??
Unadhani mungu angejidhihirisha kuna mtu angetia shaka juu ya uwepo wake?? kwa nini asijionyeshe wazi kabisa, macho ya damu na nyama yamuone ili aweze kupata uaminifu kutoka kwa wanadamu?? mtasema itaharibu uwezo wa kuchagua, lakini si anataka tumchague yeye?? akijionyesha wote si tutamchagua yeye??
zipo nyingi, ila ntazidi kuongezea kama kuna watu watauliza chochote. Acha niishie hapa....
@Gily