Mfahamu malkia victoria wa Uingereza

Anonymous

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
515
Reaction score
143
Points
0
1713332317998.png

Ukimtoa Malkia Elizabeth II basi hakuna kiongozi mwengine wa kifalme aliyeiongoza uingereza kwa miaka mingi zaidi kumzidi Malkia Victoria kwa miaka 64 ....Ndio malkia Victoria ndio jina Lake limepewa ziwa la Victoria linalopatikana hapa afrika ya mashariki ....jina lake kamili aliitwa Alexandrina Victoria

Malkia Victoria aliipigisha hatua kubwa himaya ya Uingereza katika nyanja mbali mbali kuanzia kisiasa, kiuchumi, na kijamii

- Alianza kutawala mwaka 1837 akiwa na miaka 18 ambapo alirithi uongozi kutoka kwa mjomba wake William IV.

- Alikuwa na uwezo wa kuongea lugha zaidi ya moja kingereza, kijerumani, kilatini, kifaransa, kihindi, na kiitalia

-Katika utawala wake ndio miti ya Christmas ilivyopata umaarufu
-Ni mama wa watoto 9 aliozaa na mume wake mwana wa mfalme Albert watoto hao ni Victoria, Edward, Alice, Alfred, Helena, Louise, Arthur, Leopold and Beatrice.

- Katika utawala wake ndio mapinduzi ya viwanda yalivyopata kasi zaidi ... Haya mapinduzi ya viwanda ni mojawapo ya sababu iliyoifanya uingereza kuwa hapo ilipo sasa... Kwa sababu kupitia mapinduzi hayo maisha ya watu wa uingereza yaliboreka zaidi kwan makampuni yalitengenezewA mazingira ya kuwalipa vyema wafanyakazi wao na pia kuwapa huduma muhimu kama shule na makazi

-Alinusurika idadi kubwa ya majaribio yakuuwawa Zaidi ya majaribio 8 ya kuuwawa

- Chini ya utawala wake aliweza kuitanua himaya yake sehemu mbalimbali duniani kama Australia, New Zealand, Canada, South Africa and India.

- Ni katika utawala wake ndio aliboresha mifumo ya elimu na kusitisha biashara ya utumwa

-Ni katika utawala wake walifanya marekebisho mengi ya sheria yakiwemo ya kibiashara... Yaliyoweza kuwapa nguvu wafanya biashara wa kiingereza kufanya biashara kimataifa huku wakiwa wanalindwa na sheria

-Kwenye utawala wake ndio aliboresha miundo mbinu ya uingereza ikiwemo reli na meli pia mawasiliano yaliboreshwa kama simu, telegraph hata picha pia
 
Watu wanaliona ziwa Victoria ila wengi hawajui lilikuwa named after this queen.

Nikija kuwa raisi ziwa hili nitalibadilisha jina marufuku kuitwa ziwa Victoria
 
Watu wanaliona ziwa Victoria ila wengi hawajui lilikuwa named after this queen.

Nikija kuwa raisi ziwa hili nitalibadilisha jina marufuku kuitwa ziwa Victoria
yeah unabadili tu ila ishu upande wa kenya na Uganda
 
Aise wazungu wametusaidia kutupa jina zurii sana ziwa letuuu, mkuu ungetupa na vigezo vya kuwa malkia wa uingereza, kuna binti hapa anajua lugha 2..
 

Similar threads

Mfahamu Mmiliki na Mwanzilishi Wa simu za Tecno na Infinix Siku zote lipo tumaini katika hali yeyote mtu anayokutana nayo Maishani. Umasikini au hali ngumu ya Maisha sio vitu anavyodumu navyo mtu siku zote. Nnamdi Ezeigbo, ndie Mwanzilishi na mtendaji mkuu (CEO) wa kampuni maarufu ya Slot...
Replies
6
Views
263
Habari zenu.. Nabii GEOR DAVIE Alizaliwa singida,April 25 1965 ni nabii,mwana muziki,mwandishi,mfadhili,mwanzilishi na kiongozi mkuu wa kanisa la NGURUMO YA UPAKO.. ELIMU:=. Alizaliwa na dkt.moses kasambale na phoebe,baba yake alikuwa daktari wa binadamu. Alikulia singida na baadaye...
Replies
24
Views
433
Kama ulikua humjui vizuri Mohammed Dewji 'MO' wacha nikufahamishe,"" Jina lake halisi anaitwa Mohamed Gulamabbas Dewji, Amezaliwa tarehe 8 mwezi May mwaka 1975, Mohamed Dewji amezaliwa IPEMBE mkoani SINGIDA, Ni mtoto wa pili miongoni mwa watoto sita, Wa Mzee Gulamabbas Dewji na Zubeda Dewji...
Replies
56
Views
822
Back
Top