Mfahamu Mmiliki na Mwanzilishi Wa simu za Tecno na Infinix

Anonymous

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
515
Reaction score
143
Points
0
Mfahamu Mmiliki na Mwanzilishi Wa simu za Tecno na Infinix
1694641102984.jpg

Siku zote lipo tumaini katika hali yeyote mtu anayokutana nayo Maishani. Umasikini au hali ngumu ya Maisha sio vitu anavyodumu navyo mtu siku zote.

Nnamdi Ezeigbo, ndie Mwanzilishi na mtendaji mkuu (CEO) wa kampuni maarufu ya Slot System Limited na pia Mwanzilishi mwenza wa (Co-founder)wa kampuni ya simu ya Tecno na Infinix moja ya simu zinazouza sana na kukua katika soko la Afrika.

Kutoka katika kutafta kazi bila mafanikio ikamplekea Nnamdi kuwa fundi wa kompyuta kwenye kichumba kidogo huko Nigeria. Biashara ikakubali, leo ni moja ya mifano kwa vijana wengi wa Naijeria na Afrika kwa Ujumla.

Mafanikio yake yamethibitisha kile wasemacho walimwengu, fursa inapokutana na maandalizi, mafanikio ni hutokea.

JINSI ALIVYOANZA
1694641118107.jpg

Nnamdi Ezeigbo ni asili yake ni Umahia jimbo la Abia, alizaliwa tarehe 04/08/1966 jimbo la Delta Nchini Nigeria. Baada ya masomo ya sekondari alijiinga na Chuo cha Teknolojia cha Yaba mwaka 1988, ambapo alisoma Asta-shahada (Diploma) ya uhandisi wa vifaa vya umeme (Elecronical Elecronics Engeneering).

Kati ya mwaka 1996 na 2001 alijiunga na Chuo kikuu cha Lagos ambapo alisoma Shahada ya uhandisi wa kompyutana Elecronics akahtimu na Upper Second Class, Baada ya kumaliza masomo ya diploma Nnamdi Ezeigbo alitafta kazi bila Mafanikio na mwishowe aliamua kijiajiri kama fundi wa kompyuta. Ukarimu, kujali wateja kulimpa umaarufu na kumtunuku wateja wengi sana.

KONA YA MAFANIKIO

Siku moja mteja wake wa siku nyingi alifika katika kibanda chake cha kitengenezea kompyuta, huyu mteja akamwambia angependa apanue eneo lale la biashara ili wateja wapate huduma nyingi zaidi za kompyuta, huyu mteja alimletea printer ili awe anaziuza, hiyo ilimpelekea Nnamdi kuanzisha duka lingine kwaajili ya kuuza kompyuta na vifaa vyake. Biashara ikakubali ikakua na hapo wateja wakaanza kuhtaji na bidhaa za simu.

Bwaba Nnamdi Ezeigbo akaiona fursa mpya akaongeza bidhaa za simu na simu katika duka lake. Duka hili lilikuwa maarufu kwa jina la slot.

Akiwa hana taaluma ya kuendesha biashara kubwa Nnamdi aliamua kujiunga na Shahada ya Uzamili katika masomo ya biashara (MBA program) katika Chuo kimoja cha biashara Lagos huku akihudhuria mafunzo mbalimbali ya Ujasiliamali. Miaka mi 5 baadae SLOT ilikua na lilikuwa ni jina maarufu karibu Nchi nzima wakiwa kama wauzaji wa simu za rejareja (retailer Sellers).

Kutokana na kukua mawasiliano ya simu za mkononi (Mobile phones) ilikuwa ni fursa kubwa katika soko la Nigeria lakini huduma hafifu za mitandao ilipelekea Wanaijeria wengi kununua simu zaidi ya moja ili mtandao mmoja unapokuwa na tatizo aweze kutumia mtandao mwingine.

Nnamdi aliona hili ni tatizo hivyo aliamua kufanya mawasiliano na kampuni ya Nokia akiwashawishi watengeneze simu za laini mbili kwa ajili ya soko la Nigeria, walikataa kwakuwa kwao watu kununua simu zaidi ya moja ilikuwa ina maanisha biashara.

Kupitia Mahojiano yake na "Nairametrics" NNAMDI alisema
"Hivyo nilienda China, nikakuatana na Bwana mmoja aliewahi kufanya kazi katika kampuni moja iliyojulikana kama Bird. Bird ni watengenezaji wa simu, walipata mtikisiko wakapoteza hisa zao sokoni"

Anaendelea "Hivyo nilipokutana na huyu Bwana nilimuomba tufanye kitu. Nilibuni jina na nikaisajiri, nanikaja na yule bwana hapa Nigeria, hiyo ilikuwa ni mafanikio ya hali ya juu ya biashara yetu. Tulikuja pamoja na nikabuni simu ya kwanza ya tecno, Tecno T101. Tulianza lakini soko halikutukubali lakini pia tulikuwa na tatizo kwa upande wa laini mbili hazikuwa zikifanya kazi kwa wakati mmoja, hivyo ilitupasa kufanya marekebisho tukaja na tecno T201 na kwa kiasi ilikubalika sokoni. Na kwakweli tulikuwa tukiwapa wauzaji kwa mkopo hii simu na wanapouza ndipo hutulipa, nami nilikuwa nikigharamia utengenezaji wake mwenyewe".

Nnamdi Ezeigbo, anasema kwakuwa alikuwa akigharamia mwenyewe uzalishaji wa simu alipata ugumu kuzalisha simu nyingi za kupeleka sokoni mpaka pale soko lilipoanza kukubali bidhaa zao ndipo alibadili mfumo kutoka kuziuza kwa mkopo na sasa wauzaji na wasambazaji walipaswa kununua kwa oda maalumu. Anasema "We started Using their money to order the products, this was around 2007" (Tulianza kutumia pesa zao kuagiza bidhaa, hii ilikuwa kwenye mwaka 2007).

MAFANIKIO YA TECNO NA KUIBUKA KWA SIMU NYINGINE YA INFINIX

Nnamdi katika mahojiano yake na Nairametrics alinukuliwa akisema "Kama nilivyosema, Tecno ni mwanangu na tumekua tukikua. Nilijua ipo siku watu wa daraja la kati wangeikubali tecno. Mwanzo ilikuwa simu ya watu wa kipato cha chini lakini kutokana na maboresho yetu na kuupangilia vizuri mchezo watu wa daraja la kati waliikubali na uchumi uliposhuka mwaka 2008 ilisaidia tecno kwenda katika mafanikio.

Nguvu ya manunuzi ya pesa ilishuka, hii iliwafanya watu kutafuta kitu chenye nguvu sawa lakini nafuu, hivyo kwa kiasi cha Naira 15,000 uliweza nunua Smartphone. Ahsante Mungu kwa mtandao wa 3g kwa hakika uliisaidia tecno kukua, Hivyo wanafunzi ambao hawakuweza kununua Smartphone kwa Naira 30,000 waliweza nunua kwa N15,000 na kufurahia sifa zilizo ndani ya Smartphone kama Facebook, Twitter, Whatsapp n.k" alisema Bwana Nnamdi.

Akizungumzia kuanzishwa kwa simu nyingine yenye jina la Infinix alisema, "sasa tecno imezaa Infinix, unaweza kuona jinsi tecno ilivyobadilika, na kwakuangalia haraka unaweza kuona kuwa itafika siku Tecno itatumiwa na watumiaji wa juu kabisa (Premium Customers)".

Leo tecno na Infinix ni simu zinazouza sana Nigeria na sehemu kubwa ya Afrika zikiwa na wapenzi, umaarufu na heshima kubwa kwa watumiaji wake.

Pamoja na stori hii ya kuvutia ukweli ni kuwa ukinunua Tecno au Infinix na hata Itel umenunua kampuni moja inayomilikiwa na Muafrika Nnamdi Ezeigbo.

Kampuni yake ya SLOT ina matawi zaidi ya 40 nchi nzima ya Nigeria, kwasasa Bwana Nnamdi Ezeigbo anaendesha programu za ujasiliamali katika Chuo Cha Harvad (Harvad University)
 
Namm nmegundua sifai kuajiriwa nafaa kuajiri watu
 

Similar threads

Ukimtoa Malkia Elizabeth II basi hakuna kiongozi mwengine wa kifalme aliyeiongoza uingereza kwa miaka mingi zaidi kumzidi Malkia Victoria kwa miaka 64 ....Ndio malkia Victoria ndio jina Lake limepewa ziwa la Victoria linalopatikana hapa afrika ya mashariki ....jina lake kamili aliitwa...
Replies
3
Views
565
Habari zenu.. Nabii GEOR DAVIE Alizaliwa singida,April 25 1965 ni nabii,mwana muziki,mwandishi,mfadhili,mwanzilishi na kiongozi mkuu wa kanisa la NGURUMO YA UPAKO.. ELIMU:=. Alizaliwa na dkt.moses kasambale na phoebe,baba yake alikuwa daktari wa binadamu. Alikulia singida na baadaye...
Replies
24
Views
433
Kama ulikua humjui vizuri Mohammed Dewji 'MO' wacha nikufahamishe,"" Jina lake halisi anaitwa Mohamed Gulamabbas Dewji, Amezaliwa tarehe 8 mwezi May mwaka 1975, Mohamed Dewji amezaliwa IPEMBE mkoani SINGIDA, Ni mtoto wa pili miongoni mwa watoto sita, Wa Mzee Gulamabbas Dewji na Zubeda Dewji...
Replies
56
Views
823
Back
Top