Mfahamu Mohammed Dewji (MO)

Anonymous

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
515
Reaction score
143
Points
0
Kama ulikua humjui vizuri Mohammed Dewji 'MO' wacha nikufahamishe,""

Jina lake halisi anaitwa Mohamed Gulamabbas Dewji,
Amezaliwa tarehe 8 mwezi May mwaka 1975,
Mohamed Dewji amezaliwa IPEMBE mkoani SINGIDA,
Ni mtoto wa pili miongoni mwa watoto sita,
Wa Mzee Gulamabbas Dewji na Zubeda Dewji,
Alisoma elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Arusha,
Baadaye akasomea elimu ya sekondari,
Katika Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam,

Shule hii ndio shule yene ada kubwa kuliko shule zote nchini TANZANIA,
Mwaka 1992 Mohamed Dewji alienda nchini marekani kumaliza masomo ya sekondari,
Ambapo huko alifikia katika jimbo la Florida,
Alipomaliza alijiunga elimu ya chuo kikuu hukohuko marekani,
Ambapo alisoma chuo kikuu cha GEORGETOWN,
Kilichopo jijini WASHINGTON DC na kuhitimu mwaka 1998,
Akiwa hapo alisomea shahada ya kwanza katika biashara ya kimataifa na fedha na masuala ya dini pia,
Miongoni mwa watu mashuhuri waliosomea chuo kikuu hicho ni rais mstaafu BILL CLINTON,
Pia amesoma rais wa zamani wa Ufilipino GLORIA ARROYO,
Lakini pia Mfalme wa JORDAN aitwae ABDULLAH,
NAa wachezaji mbalimbali wa NBA kama vile ALLEN IVERSON na PATRICK EWING,

Mohamed Dewji baada ya kuhitimu alirejea Tanzania,
Na kuanza kushiriki katika usimamizi wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL),
Kampuni ambayo imeanzishwa na babake miaka ya 1970,
Katika kampuni hiyo Mohamed Dewji alihudumu kwa miaka miwili kama mfanyakazi wa kawaida,
Kabla ya kuwa afisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo,
Wadhifa ambao ameendelea kuushikilia hadi sasa,
Mohamed Dewji ndiye tajiri namba moja Afrika Mashariki,
Na pia yupo miongoni mwa matajiri wenye umri mdogo zaidi Afrika.

CHANZO CHA UTAJIRI WA MO

Kampuni ya METL ilifanikiwa kwa kununua viwanda vya nguo na mafuta,
Vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo sana,
Na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa wa menejimenti,
Kwasasa METL ina viwanda vya kutengeneza nguo,
Na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji,
Pia ina mapato yanayozidi Dola za kimarekani milioni 1.4 milioni kwa mwaka,

Katika kampuni hiyo ambayo imekuwa na ushindani,
Dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa,
Mohamed Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote,
Kwa mujibu wa tovuti yake METL inaendesha shughuli za uagizaji na usafirishaji bidhaa,
Kutoka na kwenda nje ya nchi ya Tanzania,

Bidhaa zinazo husiana na nguo, vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati, petroli na utengenezaji baiskeli,
Pia METL inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo,
Na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam,

Kampuni ya METL inafanya shughuli zake katika nchi nyingi barani Afrika,
Kama vile Tanzania, Uganda, Sudan Kusini, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Malawi, Msumbiji na Zambia,
Ambapo kwasasa ina wafanyakazi zaidi ya 28,000,
Shughuli za METL huchangia 3.5% katika pato la taifa (GDP) la Tanzania,
Kiwango cha wastani cha ukuaji wa mapato ya kampuni hiyo kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2014,
Ilikua dola milioni 30 hadi Dola bilioni 1.3,
Ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 200%,
Mohamed Dewji ame orodheshwa kuwa tajili wa 17,
Kwenye orodha ya mabilionea barani Afrika,
Na wa 1561 duniani kwenye orodha ya mabilionea mwaka 2018,
Wakati fulani kampuni ya METL ilianzisha kinywaji kiitwacho Mo Cola kushindana na Coca Cola,
Mohamed Dewji ndio Mtanzania pekee hadi sasa,
Aliyesaini mkataba mwaka 2016 wa kutoa kwa wahitaji nusu ya mali yake,
Mkataba huo ulisainiwa baada ya mwaka 2014,
Mohamed Dewji Foundation kuanzishwa,
Ili kutekeleza nia yake hiyo na kazi yake kubwa ni kusaidia watanzania wasiojiweza,
Kwa upande wa afya, elimu na maendeleo jamii.

SIASA

Mbali na biashara na shughuli za jamii Mohamed Dewji,
Amewahi kuwa mwanasiasa hiyo ilikua mwaka 2005 mpaka 2015,
Ambapo Mohamed Dewji alikuwa mbunge wa Singida Mjini,
Alijiingiza katika siasa mara ya kwanza mwaka 2000,
Ambapo alishinda uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo hilo,
Wakati huo akiwa na miaka 25 lakini akazuiwa kuwania ubunge,
Kwa madai kwamba alikuwa bado mdogo kiumri,
Baadae ilipofika mwaka 2015 aliamua kustaafu siasa,
Na kuamua kujikita zaidi kwenye biashara tu,
Mwaka 2015 alitajwa kuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi Afrika,
Na jarida la Forbes na baadaye akatawazwa mtu Mashuhuri wa Mwaka wa Forbes,
Mwaka uliofuata alishinda tuzo ya Afisa Mtendaji mkuu bora wa Mwaka Afrika,
Katika mkutano mkuu wa maafisa watendaji wakuu Afrika.

FAMILIA

Mohamed Dewji ameoa mke anaitwa SAIRA,
Mwanamke aliyekuwa anapendana nae tangu utotoni,
Na wamejaliwa watoto watatu waitwao NYLA, ABBAS na MAHDI,
Baada ya kufunga ndoa mwaka 2001,
Mohamed Dewji na mke wake walikutana Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam.

MICHEZO

Mohamed Dewji ni mpenzi wa michezo na shabiki mkubwa wa Simba,
Na amewekeza katika klabu ya mpira wa miguu iitwayo Simba Sports Club.

SABABU YA KUREJEA TANZANIA KUTOKA MAREKANI

Mohamed Dewji alisomea Marekani na mpango wake ulikuwa kusalia na kufanya kazi huko,
Mwezi Septemba mwaka 2018 aliandika kwenye Instagram sababu iliyomfanya kurejea,
Ambapo anasema;- Ni ushauri wa baba yake pamoja na kugundua kwamba kulikuwa na fursa nyingi Tanzania.

UJUMBE ALIOUANDIKA TAREHE 10 SEPTEMBA MWAKA 2018.

Aliiandika hivi:- "Nilipomaliza masomo yangu ya shahada nikiwa nchini Marekani niliamua kubaki huko na kufanya kazi,
Nilitumia muda na nguvu nyingi kazini lakini pesa ambayo niliipata haikukidhi kufanikisha malengo yangu,
Ndipo baba yangu akanishauri nirejee nyumbani Tanzania,
Na nilipofatilia kwa kipindi hicho niligundua kwamba,
Nchini Tanzania kuna fursa nyingi za kibiashara,
Na hapo ndipo nilipo amua kurudi na kujiunga katika biashara ya familia,
Muhimu kufahamu ni kwamba mafanikio sio lazima uende kuyatafuta nje ya nchi,
Hapa hapa nchini kwetu kuna fursa ambazo ukifanyia kazi utafanikiwa,
Unafikiri kwanini baadhi ya watu wanapenda kuishi/kufanya kazi nje ya nchi?".... alisema Mohamed Dewji.
 
Last edited by a moderator:
jifunze kukwepa kodi na kuhonga wanasiasa kaa unataka kua bilionea, code hazitokubeba😂
Nakwepa code kwa biashara gani niliyonayo?
Na huyo mwanasiasa namuhonga kikombe cha kahawa au?
 
Nakwepa code kwa biashara gani niliyonayo?
Na huyo mwanasiasa namuhonga kikombe cha kahawa au?
hapo sasa.... we jua tu kuwa bilionea itabidi ufanye vitu vibaya mahali.... kutokulipa watu, kukwepa kodi, wizi.... n.k
 

Similar threads

Ukimtoa Malkia Elizabeth II basi hakuna kiongozi mwengine wa kifalme aliyeiongoza uingereza kwa miaka mingi zaidi kumzidi Malkia Victoria kwa miaka 64 ....Ndio malkia Victoria ndio jina Lake limepewa ziwa la Victoria linalopatikana hapa afrika ya mashariki ....jina lake kamili aliitwa...
Replies
3
Views
565
Mfahamu Mmiliki na Mwanzilishi Wa simu za Tecno na Infinix Siku zote lipo tumaini katika hali yeyote mtu anayokutana nayo Maishani. Umasikini au hali ngumu ya Maisha sio vitu anavyodumu navyo mtu siku zote. Nnamdi Ezeigbo, ndie Mwanzilishi na mtendaji mkuu (CEO) wa kampuni maarufu ya Slot...
Replies
6
Views
264
Habari zenu.. Nabii GEOR DAVIE Alizaliwa singida,April 25 1965 ni nabii,mwana muziki,mwandishi,mfadhili,mwanzilishi na kiongozi mkuu wa kanisa la NGURUMO YA UPAKO.. ELIMU:=. Alizaliwa na dkt.moses kasambale na phoebe,baba yake alikuwa daktari wa binadamu. Alikulia singida na baadaye...
Replies
24
Views
433
Back
Top