Leo ningekuwa kijana .
Haki nisingewaza kuajiliwa ila ningepambana nipate mtaji nifanye biashara binafsi kwa kujikongoja , je unajua kwanini ? Ndugu zangu hela ya kupokea baada ya siku kadhaa ni mbaya sana inadumaza ubongo , fikra na mipango .
Utasema kwanini ? Ni pale utachezea hela au utajiona Don kwasababu unajua mwisho wa mwezi utaingiza tena kiasi kingine ila ukiwa hauna hesabu ya mwisho wa mwezi kwa unayejielewa utaiheshimu hela .
Ila nikukumbushe kuwa hela ya kushika kila siku hata kama ni elfu moja ni tamu sana kuliko ya kusubiri uingiziwe mwisho wa mwezi , unauliza kwanini ? Wafuatilie wafanyabiashara wa kati na wadogo wengi wana nuru usoni , afya nzuri kiasi chake alafu njoo kwa wenzangu na mimi akina mwalimu , bwana daktari , askari na bwana mifugo wengi ukikaa naye kwa muda utagundua anafosi tabasamu ila yamemjaa .
Narudia tena , wengi wanaosubir mwisho wa mwezi daima uanza kunawiri na kuonekana maisha kayapatia baada ya kujenga nyumba kwa mkopo , kuwa na kigari cha mkopo na hapo akafungia kabiashara ambako uwa hakadumu kanapotea kwa walio wengi , sasa jiulize kwanini uanza kunenepa na kuonekana maisha wameyapatia .
Ndugu ukweli ni kuwa ukiwa unatoka kwenye familia za umasikini sana jambo la kwanza kupambana nalo ni ukombozi wa fikra na mawazo aisee ukijikuta bado unahisi kumiliki gari ni utajiri , mara gari aisee bado unaziishi mindset za kwenu huko umasikinini kwahivyo walio wengi wanaopokea mishahara uanza kunenepeana na kunawiri baada ya kumiliki huto tu vitu ni hapo mtu kwa kumiliki kagari ka mkopo na kanyumba kwa mkopo wa milioni 19 basi mindset yake umtuma kuwa katoboa tayari ni hapo anakuwa anaona kila kitu kipo sawa .
Maana hela ukatwa direct huko kwenye kamshahara sasa kichekesho uwa ni kwenye tugari wanatonunua maana hata kuafford kuyaendesha mwez mzima uwa ni shughuli pevu .
Itoshe kusema mshahara haujawahi kutosha na hautotosha ila kujiwekeza ni muhimu ila asikudanganye mtu hela ya day to day ni tamu sana maana kwako neno dharura ni la mara chache tofauti na wenzangu na mimi wao kila wakienda kukopa hawaishi kusema dharura