PESA SIO KILA KITU KWENYE MAPENZI

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

The great manenge

New member
Platinum Villager
Joined
Jul 8, 2023
Messages
1,320
Reaction score
2,995
Points
0
Ukitembea na kuzungumza na vijana wengi wa sasa wanakuambia ukiwa na pesa ‘utang’oa’ demu wa aina yeyote, kwa sababu huwa hawana ujanja panapo mapesa. Na hili linadhihirishwa na wengi wanapobadili wanawake kwa sababu ya uwezo wao wa kifedha.
Na hata wanawake wenyewe nao wanaonekana kuhamasika sana kukutana na mvulana mwenye fedha, kama ambavyo hata vijana wa kiume nao siku hizi hupenda wadada wenye nazo.
Lakini ninataka kusema jambo moja ili kila mmoja limkae akilini mwake, kwamba pamoja na ukweli huu wa fedha kuchagiza sana mapenzi, lakini mapenzi ya kweli yapo na yana nguvu kubwa kuliko kawaida.
Uthibitisho wa hili, chunguza au jichunguze mwenyewe unapofuatilia penzi la pesa. Kwa wavulana, wana pesa, wana mke nyumbani (wanayempenda) utawasikia wanatamka maneno kama haya “leo nataka mlupo wa maana nikapumzike nao”
Na akina dada nao, wanaoishi na waume wawapendao unaweza kuwasikia wakisema “Sijui nimpate wapi zoba ajiingize nipate hela ya saluni.”Maana ya kauli ya wawili hawa ni kuwa wako tayari kutumia au kutumiwa na fedha ili kukidhi matamanio yao ya kimwili na kimahitaji. Mvulana atataka aifurahishe nafsi yake kwa kumpata msichana kwa fedha, wakati mdada atahitaji fedha kwa kuutumia mwili wake ili mradi tu apate kutimiza mahitaji yake.
Lakini jambo tunaloweza kujifunza ni kwamba wote wana wenza wao ambao hawahitaji fedha ili kufurahi nao. Wanaume wenye wapenzi wao, huogopa kuwapa fedha zenye mlengo wa kuhonga.
Pesa hutajwa kwenye maendeleo baina ya wawili na siyo mtaji wa kumalizana kiu ya kimahaba. Unaweza kumkuta msichana mrembo anatoka na mtu mwenye fedha, lakini ukimchunguza undani wake, unakuta kuwa huko anakotoka, anaye mpenzi wake wa dhati kabisa, ambaye wakati mwingine huwa anaelewa uhusiano wa mpenziwe huyo na kibopa.
Ninachotaka wote kuamini ni kuwa hakuna kiwango cha fedha kinachoweza kununua mapenzi, isipokuwa mapenzi ya dhati yanaweza kukusanya kiasi chote cha fedha kilichopo na kukileta ndani.
Pesa ni mbwembwe tu, lakini hazina ubavu wowote wa kudhibiti penzi. Ndiyo maana unawaona wanawake walioolewa na matajiri wanatoka nje, tena na magari yenye vioo vya giza, wanaenda kuupa moyo burudani huko kusiko na fedha.
Msichana atakimbia ndoa ya kijana wa bilionea, atafurahia kuishi na mwenza wake hohehahe, ili mradi tu, nafsi yake inapata burudani iliyokusudiwa.Hujaona watoto wa kike wakijinyonga kwa kukataa ndoa za lazima? Hii ni kwa sababu wazazi wameshachukua ng’ombe na hela, lakini upendo wa binti uko kwa mtu mwingine kabisa, ambaye wakubwa hawamtaki kwa vile hawezi kutoa mahari kubwa
 

Similar threads

Habari.. Kama kichwa kinavyojieleza chenyewe. Kiasi gani cha fedha uliwahi kushika katika maisha yako. Hapa nataka pesa zako kwa jasho lako wewe mwenyewe sio za kupewa na wazazi wako au ndugu zako au marafiki zako nataka cha kwako pekee yako. Mimi nimeshawahi kushika 15 millions kwenye...
Replies
58
Views
941
Nina maana ukipata watu 20 au 30 kila siku mtu mmoja anatoa 5000 au 10000 na kila siku mtu mmoja anatoka. Siitatusaidia kidogo kupambana na maisha. Wewe ni prezidaa uwezi kimbia ukaacha app
Replies
102
Views
2K
Wakuu kwema? Binafsi yangu kuwaeleza watu kuhusu mipango yangu naona sio sawa maana watu niwajuaji sana wanaweza wakaanza kukushauri negatively au kukukatisha tama...
Replies
13
Views
762
Wengi hawajapata kufahamu kuwa wanawake pia hupatwa na ugonjwa wa mabusha.
Replies
7
Views
216
Katika moja na mbili Jumamosi usiku mwingi sana chimbo flani la walesa mavi, kula vombo kula vombo kula vombo mpaka natambaa, kudadeki wasela mavi wakasepa na kisimu changu cha kutambia mjini pumbavu zao. Nililia kisenge! Silewi tena.
Replies
95
Views
1K

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top Bottom