TAFSIRI YA NDOTO

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,883
Reaction score
3,969
Points
113
Habari za wakati huu.. natumai haujambo, hata mimi niko salama sana..

Nimeanzisha uzi huu ili kujaribu kutoa tafsiri ya ndoto zako KIBIBLIA..

Kwahyo nakaribisha yeyote kushare ndoto yake hapa na mimi nitajitaidi kukupa tafsiri yake sawasawa na neno, kumbuka biblia ina kila kitu na ndio ntakayokua naitumia kutafsiri kila ndoto utakayo weka hapa..

Pia ntaendelea kuanda na kuweka hapa maana ya ndoto, aina za ndoto, ukiota ufanye nini nk.
Karibuni
 
Huwa naota ndoto niko high school kipindi cha mitihani
Ujaeleza kwa upana, ulikua unafanya mitihani au ilikua kipindi cha mitihani? Ulifanikiwa kuifanya?
 
Nimeota nilikuwa natafuta sana maziwa Ila hayakuwa yanapatikana baada ya kuchoka kutafuta maziwa nilikaa nje nione kama wangepitisha. (Maziwa hayakuwa yanapatikana kwa muda mrefu kama miezi hivi)

Baadae akatokea mtu anapitisha akaja kwangu akasema nimekuletea maziwa uliyokuwa unatafuta, nikafurahi ☺️

Hii inamaana? Naomba niambie kama unajua
 
Ina maana, ntaiweka hapa soon
 
Kwa ujumla ujumbe umekuja ili usikate tamaa kwa yale mambo mazuri ulikua unayatamani au kuyasubiri...

Inaonesha utapata external support (kimwili au kiroho) itakayo kubadilisha hali yako nakua huru zaidi, nguvu zaidi, afya zaidi, hatua zaidi, furaha zaidi au kipato zaidi.

Inaweza kua kinyume chake pia pengine kuna mtu wako wa karibu anaitaji care yako ili aweze kufika mahali pazuri.

Mara nyingi katika biblia maziwa yana maanisha Neno(kumbuka neno linakuweka huru), maziwa yana maanisha utele na afya(nchi ya maziwa na asali), kwa maelezo yako neno hili litakufaa sana kwa tafsiri ya ndoto yako 👇👇

1 Petro 2:2
Kama vile watoto wachanga wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswa kuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua na kukombolewa.( bibilia habari njema)

Kwa nguvu ya maziwa mpate kukua na kukombolewa( haya maneno hayana tofauti na nilivo toa maelezo kuwa utapata suport na itakuvusha kinamna flani)
Nadhani utakua umepata kitu February girl
 
Nashukuru sana kwa tasfiri...

Mara nyingi naota ndoto za mambo yangu mwenyewe na ndoto zangu hutokea kweli lakini hii imekuja kimafumbo kidogo. Nashukuru kwa tasfiri ngoja nisubiri maziwa 🤩🤩
 
Sehemu ya pili

Vyanzo vya ndoto

Kwakuzingatia title na lengo la uzi huu "Tafsiri ya ndoto" kuna aina mbili ya vyanzo vya ndoto.
Kuna ndoto kutoka kwa Mungu na kuna ndoto kutoka kwa shetani

Japo kuna vyanzo vingine vya ndoto kwa mfano ndoto zinazoletwa na ubongo na shughuli nyingi. Mara nyingi zinakua hazina maana kwakua ni mfululizo wa picha au matukio yanayo chakatwa na ubongo (mhubiri 5:3,Isaya29:8)..

Ndoto zinaweza kuja moja kwa moja yaani zinaeleweka haziitaji kutafsiri mfano Mathayo 2:13 Yusufu anapata maelekezo ya kwenda Misri, ndoto hii ilikua imejitosheleza inaeleweka bila tafsiri..

Pia kuna ndoto zinazokuja kwa mafumbo na zinaitaji tafsiri kwakua ningumu kuelewa aina ya lugha ishara alama zilizo tumika,,

Kumbuka Roho mtakatifu anauwezo wa kufumbua mafumbo yote, haijalishi chanzo cha fumbo ni shetan au Mungu..

Watu wengi wamekua wakipata ndoto zenye mafumbo na wakashindwa kuelewa nini maana ya ndoto husika na ndio maana nmejaribu kuandika uzi huu ili tupate kujua tafsiri kupitia neno la Mungu..

Kumbuka ndoto ni halisi zaidi maana mtu ni roho na mambo yote ya mwilini yanaanzia rohoni, kila tukio na jambo lolote unaloliona na kulijua chanzo chake ni rohoni...

Lengo la ndoto

Ndoto utumika kama mawasiliano ya mtu na ulimwengu wa roho, kumbuka mtu ni roho.

Mungu utumia ndoto kujulisha watu: Kusudi la wao kuwa duniani(purpose of life) na kujulisha mambo yajayo 👉Mwanzo 41, kuwaonya👉 Mwanzo 20:3, kuwalinda👉Mathayo2:13 , kuwapa taharifa au uthibitisho 👉Mathayo 27:17-19,
Kuwafundisha, kuwafariji, kuwaponya, kuwa sahihisha nk.

Shetani anaweza kuleta ndoto kwa watu pia kutaka kupitisha ajenda zake( Yuda1:8, K.torati13:1-5

Kitu kingine unachotakiwa kujua ni kwamba ndoto anaweza pata mtu yoyote hata kama ni mpagani...

Itaendelea
 
Similar threads

Kila mtu na kile akipendacho je wewe unapenda simu ya namna gani na unawish ukiipata tu roho itatulia?
Replies
42
Views
660
Back
Top