KUTOKA KATIKA MAANDIKO MATAKATIFU NENO LA MUNGU LA SIKU

Urban Edmund

New member
Platinum Villager
Joined
Jun 26, 2023
Messages
636
Reaction score
1,321
Points
0
Hapa unaandika neno unalolipenda kutoka katika biblia

Yeremia 29:11-13 BHN​

Maana, mimi Mwenyezi-Mungu ninajua mambo niliyowapangia. Nimewapangieni mema na si mabaya, ili mpate kuwa na tumaini la baadaye. Hapo ndipo mtakaponiita na kuniomba, nami nitawasikiliza. Mtanitafuta na kunipata. Mtakaponitafuta kwa moyo woteimages (19).jpeg
 
UFUNUO WA YOHANA 21
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu
 
1 Kor 13:4-8 SUV
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
 
24 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Mathayo 6:24
 
Kutoka 23:5,7
[5]Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye hali ameanguka chini ya mzigo wake, nawe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.
[7]Jitenge mbali na neno uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu.
 
2 Petro 3
3 Kwanza kabisa ni lazima muelewe hili: kwamba siku za mwisho watu wenye dhihaka watakuja kuwadhihaki wakiwa wametawaliwa na tamaa zao wenyewe. 4 Watawaambia, “Aliyeahidi atakuja yuko wapi? Tangu baba zetu walipokufa mambo yameendelea kuwa kama yalivyokuwa tangu kuumbwa kwa dunia.” 5 Wao wameamua kusahau kwamba ni kwa neno la Mungu mbingu zilikuwepo tangu zamani, na kwamba ulimwengu uliumbwa kutokana na maji kwa njia ya maji, 6 na kuwa kwa maji hayo hayo ulimwengu ule uliokuwepo uliangamizwa wakati ule wa gharika. 7 Lakini kwa neno hilo hilo mbingu na dunia, ambazo zipo hivi sasa, zimewekwa akiba kuchomwa moto, zimewekwa mpaka siku ile ya hukumu na ya kuangami zwa kwa watu wasiomcha Mungu.
 
Waebrania 13
4 Ndoa iheshimiwe na watu wote, na wenye ndoa wawe waaminifu kwa wenzi wao ; maana Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati.
 
2 Petro 3
3 Kwanza kabisa ni lazima muelewe hili: kwamba siku za mwisho watu wenye dhihaka watakuja kuwadhihaki wakiwa wametawaliwa na tamaa zao wenyewe. 4 Watawaambia, “Aliyeahidi atakuja yuko wapi? Tangu baba zetu walipokufa mambo yameendelea kuwa kama yalivyokuwa tangu kuumbwa kwa dunia.” 5 Wao wameamua kusahau kwamba ni kwa neno la Mungu mbingu zilikuwepo tangu zamani, na kwamba ulimwengu uliumbwa kutokana na maji kwa njia ya maji, 6 na kuwa kwa maji hayo hayo ulimwengu ule uliokuwepo uliangamizwa wakati ule wa gharika. 7 Lakini kwa neno hilo hilo mbingu na dunia, ambazo zipo hivi sasa, zimewekwa akiba kuchomwa moto, zimewekwa mpaka siku ile ya hukumu na ya kuangami zwa kwa watu wasiomcha Mungu.
@mshamba_mkuu
 

Similar threads

Kichwa kinajieleza, Kuna baadhi ya muvie na simulizi ukiziangalia basi unajikuta umewakubali sana baadhi ya wahusika. Kwa mimi ni kama ifuatavyo: 1. Pedro Alonso/Berlin - Money heist Jamaa ana calmness, man of action, genius na yupo very cold. 2. Tommy shelby - peaky blinders Huu ni mwamba...
Replies
7
Views
377
Je pata seca ni nani?? Pata seca alikuwa mtumwa wa kiafrica aliyetoka nchi ya brazili,alizaliwa mwaka wa 1858 huko sorocoba [Sao paulo] Brazil. Jamaa alikuwa anamwili mkubwa sana alikuwa na urefu wa futi 7(2.18 meters), kipindi cha utumwa huko brazil wazungu walimpenda kwa sababu ya mwili...
Replies
5
Views
361
Je, umewahi kuthubutu kuita mzimu? Tamaduni hii ya ngano inadai kwamba ikiwa unawasha mshumaa katika chumba chenye mwanga hafifu na kuimba "boody Marry" mara 3 mbele ya kioo, utamwona mwanamke akichuruzika damu katika kuakisi. Huwa wanadai aanaweza kukupigia kelele, au hata kukutazama akiwa...
Replies
8
Views
196
  • Sticky
KITU NACHOTAKA BABA NINAHITAJI KUSOMA Hodi hodi naingia, baba bora umekuja kuna jambo kukwambia, nisikize mara moja shairi nakusomea, sikiliza zangu hoja kitu nachotaka baba, ninahitaji kusoma wala 'sinipe kibaba, na shamba la kulima eti unipe mbaba, na ndoa ya mapema so niishie la saba...
Replies
18
Views
306
Tofauti ya funzo tunalopata shuleni na lile tunalopata katika maisha; Kwanza kabisa nikusalimu wewe mpendwa wa kf ni muda sasa tangu tumeonana(kupitia madandiko), nikushukuru pia in advance kwa kunisamehe kwa mwandiko wangu, bado nadhidi kuimarika, moja kwa zote kwenye madaaa Katika maisha...
Replies
12
Views
392
Back
Top