UCHAWI upo au ni hadithi za kutungwa??

The great manenge

New member
Platinum Villager
Joined
Jul 8, 2023
Messages
1,320
Reaction score
2,995
Points
0
Wasalaaam....
Kumekuwa na imani mbalimbali miongoni mwa jamii yetu kuwa uchawi upo wengine wana imani haupo..
Je una amini uchawi upo????


Kwenye kijiji kimoja katika milima huko Scotland, Tonks Brown anasema anajivunia kuwa mchawi.

Kwake sherehe za Halloween hazihusu tu mavazi, maboga au matibabu

"Ni zaidi ya hayo: Ni sehemu kubwa ya maisha yangu, ni dini yangu na imani yangu, anasema Tonks mwneye umri wa miaka 36.

Mwaka mpya wa pagani ni Novemba mosi na Tonks anasema tarehe hiyo inaashiria mwanzo mpya.

Alibadilika na kuwa mpagani akiwa umri wa miaka 12 akiishi eneo lijulikanalo kama Isle of Mull kaskazini magharibi mwa Scotland.

"Nilionewa nikiwa shule ya sekondari kwa kuwa tofauti," anasema.

Wanililazimisha kuhudhurua kanisa la We Free Church nikiwa shuleni, kulikuwa na ibada na maombi kila wakati."

"Nakumbuka nikikemewa kwa kujichora wakati nilitakiwa kuomba."
Tuachane na Tonks...
Tuje kwenye mada yetu
.
NINI MAANA YA UCHAWI?
JIBU: Katika ukristo kitendo chochote cha kutafuta msaada wa rohoni au mwilini kwa kupitia nguvu nyingine mbali na nguvu za Mungu, biblia inakiita Uchawi,…Na ni wazi kuwa hakuna nguvu nyingine iliyo kinyume na Mungu zaidi ya nguvu za shetani, Na uchawi kwa ujumla umebeba mambo mengi, kuloga, kuagua, kutazama utabiri wa nyota, kubashiri, kusihiri, kuabudu sanamu, hata kuamini baadhi ya movie au magemu ambayo yanatoa maagizo fulani kukuaminisha kuwa unaweza kupata maelekezo ya maisha yako mbali na nguvu za Mungu ni uchawi n.k. vipo vingi, kwa ujumla vyote hivyo vinaitwa uchawi.

Uchawi ni jambo ambalo uhusishwa au kukaribishwa kwa shetani wa kijini na kutakiwa msaada kutokana na jambo hilo. Asili ya Uchawi nikubadilika kitu kutoka katika hali yake ya hakika na kwenda katika hali nyingine.

Uchawi pia huweza kukitoa kitu katika hali ya uzuri na kwenda katika hali ya ubaya au jambo ambalo uhusishwa na mambo yaliyofichika sababu zake na(kubadilisha) kubadilika kitu kutoka katika hakika yake na kupita katika mapito ya hadaa.

Uchawi inaweza ikawa ni maneno yenye kuzungumzwa au maandishi yenye kuandikwa.

Je uchawi upo???


Ushahidi katika vitabu vya dini na sheria za Nchi kama Tanzania na Ulaya
Sheria ya uchawi Tanzania inahukumu mchawi akibainika kwa ushahidi ni kifungo cha miaka 7 au chini ya hapo kutegemea madhara aliyosababisha, ushahidi ni huu hapa chini wa sheria hiyo, iko chapter ya 18 na inaitwa THE WITCHCRAFT ACT

___ CHAPTER 18 _______

THE WITCHCRAFT ACT

An Act to provide for the punishment of witchcraft and of certain acts connected therewith.

»Shetani anawasaidizi wake watendao kazi pamoja naye. Wasaidizi hawa huitwa PEPO WABAYA au MAJINI au MASHETANI. Katika biblià majina haya yote yanazungumzia jambo moja (WAEFESO 6:11-12 ; MAMBO YA WALAWI 17:7; KUMBUKUMBU LA TORATI 32:17 ; ISAYA 13:21 ; 1 WAKORINTHO 10:20-21).

»UCHAWI ni kufanya tendo la kushirikiana na pepo au majini au mashetani hawa na kuwatumia ili kuwadhuru watu wengine.

»Kazi ya Shetani ni kuchinja, kuua , kuharibu na kuibiba chochote chema tulichonacho (YOHANA 10:10).

»Pepo hawa hawaonekani kwa macho ya kawaida na tena wanaweza kupenya na kufanya makao ndani ya kiungo cha mwanadamu hata kilicho kidogo sana kama mshipa na kukiharibu.

»USHIRIKINA ni ushirikiano na MASHETANI katika kukamilisha kazi zao mbaya.

»Mtu anaweza kufanya mambo ya kushangaza yasiyo ya kawaida au asili(SUPERNATURAL) kwa kutumia nguvu za giza za Shetani au uchawi kama Simoni mchawi (MATENDO YA MITUME 8:9-11).

»Kwa kutumia nguvu za kichawi mtu anaweza KUMLAANI mtu nakupatwa na madhara. Mfano, mtu anaweza kumlaani mtu aliyemwibia fedha zake na kupatwa na madhara mpaka wakati atakapokiri kuzichukua na kuzirudisha kama alivyotendewa MIKA (WAAMUZI 17:1-2). Laana inaweza kuathiri familia nzima, ukoo na hata kizazi hadi kizazi.

»Wachawi walikuwepo tangu zamani. Kabla ya Yesu Kristo, tangu zamani za Farao wa Misri na nyakati zinazofuata wanatajwa wachawi wengi(KUTOKA 7:11; YOSHUA 13:22; 1 SAMWELI 28:9; 2 WAFALME 21:1-2,6; ISAYA 19:3; ISAYA 57:3; DANIELI 2:2; DANIELI 5:7).

»Hata baada ya Yesu Kristo, nyakati za kanisa la kwanza wachawi waliendelea kuwepo. Kulikuwepo mchawi aliyeitwa Simoni aliyekuwa akifanya uchawi katika taifa la Wasamaria(MATENDO 8:9-11). Mchawi mwingine anayetanjwa ni Bar-Yesu au Elima (MATENDO 13:6-8).

» Mungu aliweka sheria kwa lengo la kuwaondosha nyakati hizo (KUTOKA 22:18; MAMBO YA WALAWI 20:27) na akaeleza jinsi watu wake wasivyopaswa KULOGA au kufanya ushirikina na MASHETANI maana hayo ni MACHUKIZO KWA BWANA(MAMBO YA WALAWI 19:26; KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14).

»Watu wengi kwa kujifanya wako juu kiroho hukana kwamba hakuna uchawi kabisa na kufikiri kwamba kufanya hivyo ndiyo kuishikilia imani ya Ukristo.

»Kuwepo kwa uchawi ni jambo lisilopaswa kukanushwa na Mwanafunzi yeyote wa biblià.
Kwa sababu kuwepo kwa uchawi kunatajwa wazi sana katika biblià.

»Hivyo kulogwa ni jambo lililohalisi.

******Wachawi wanachukua nyota...****
Je Wanaichukuaje? kwasababu wachawi wanaweza kuiona nyota ya mtu na kuifuata, hivyo wakigundua kuwa nyota ni nzuri wanaweza kuichukua na kumuuzia mtu mwingine; na ndio maana mtu anaweza kuzaliwa nyota ya uongozi, ujasiri, upendeleo, ubunifu au kupata kibali mbele za watu, alafu ikachukuliwa na kupewa mtu mwingine. Na ndio maana kuna watu ni matajiri kwasababu ya nyota za watu; na wakati huohuo mtu Yule ambaye nyota yake oimechukuliwa anaanza kuwa na matatizo; kile kibali au upendeleo aliokuwa nao awali hawezi kuwa nao tena

Uchawi upo.........
 

Similar threads

  • Article Article
SEHEMU YA KWANZA. Nikiwa nimerudi kutoka shuleni nilikutana na mama nje ambaye alinambia tumepata mgeni ambaye atakua akitusaidia kazi za ndani yaani dada wa kazi, kutokana na uchovu na fimbo za siku hio hata sikua na hamu ya kutaka kujua zaidi kuhusu jambo hilo nilimjibu mama kwa kifupi...
Replies
63
Views
1K
Toka huu mwaka uanze nimetamani sana kumiliki uchawi,ila uchawi ninaotaka sio wa kutoa kafara,au kuua mtu. Uchawi naotaka niwakutibu watu Sitaki uchawi wa majini. Nataka uchawi wakunisaidia mimi na jamii inayonizinguka. Mfano kugundua vitu vipya Kumuweka limtu liwe linanifanyia biashara zangu...
Replies
39
Views
781
  • Article Article
Riwaya: Hadithi Zimeamshwa: Minong'ono ya Pagoda ya Mbinguni Mwandishi: King of Dragonmarsh Imetafasiriwa: Hakimu Mchapishaji: KijijiForums Aina ya Riwaya: Epic Fantasy / Mapenzi ya Kusikitisha / Drama ya Giza Onyo:Hii ni kazi ya kubuni kabisa. Isipokuwa imeelezwa vinginevyo, majina yote...
Replies
4
Views
57
Kumekuwa na watu wengi wakijitojeza wakodai kuwa kuna madhara kulala na kioo kutazama kitanda. Inaaminika kuwa kulala na kioo kutazama kitanda huleta: Mikosi, Kukosa usingizi, Kuvunjika kwa ndoa, Migogoro, Ndoto mbaya nk., Nadharia hii inatoka wapi? Dhana kwamba hupaswi kulala mbele ya kioo...
Replies
8
Views
455

Donations

Total amount
$0.00
Goal
$300.00
Back
Top