Tofauti kati ya mwanaume na mwanamke

Anonymous

New member
Joined
Jun 4, 2023
Messages
515
Reaction score
143
Points
0
Mwana saikolojia wa kimarekani, Profesa Reek amechapisha matokeo ya utafiti wake juu ya mwanaume na mwanamke katika kitabu kikubwa. Anasema: Ulimwengu wa mwanaume ni tofauti kabisa na ule wa mwanamke. Ikiwa mwanamke hawezi kufikiri au kufanya mambo kama mwanaume, ni kwa sababu wanaishi katika dunia mbili tofauti.

Ameendelea kusema kuwa; “Kwa mujibu wa Agano la Kale, mwanaume na mwanamke wametokana na mwili mmoja. Hivyo ni kweli lakini ingawa wametokana na mwili mmoja, wana miili miwili tofauti, ambayo haifanani kabisa katika maumbile yake.

Hawana hisia za aina moja na hawaonyeshi mwitikio wa aina moja katika matukio na ajali mbali mbali. Wako kama sayari mbili zinazozunguka katika njia mbili tofauti. Wanaweza kuelewana na wanaweza kukamilishana, lakini sio kitu kimoja (sawa). Hii ndio sababu wanaweza kukaa pamoja, kupendana na wanaweza wasichokane.

Profesa Reek analinganisha roho ya mwanaume na mwanamke na anagundua tofauti nyingi. Anasema; “Inakinaisha (chosha) kwa mwanaume kukaa na mwanamke anayempenda muda wote. Lakini hakuna kitu kizuri kwa mwanamke kuwa karibu na mwanaume anayempenda.

Mwanaume mara zote anataka kubaki vile vile. Lakini mwanamke anataka kuamka akiwa tofauti na mpya kila siku.

Sentensi bora kabisa ambayo mwanaume anaweza kumwambia mwanamke ni kuwa ‘Mpenzi wangu, nakupenda.’ Sentensi nzuri kabisa ambayo mwanamke hupenda kumwambia mwanaume ni, ‘Naona fahari kuwa na wewe.’

Mwanaume aliyepata kuwa na wanawake wengi katika maisha yake huwavutia sana wanawake wengine. Lakini wanaume hawapendi wanawake waliopata kuwa na wanaume wengine huko nyuma.

Wanaume wanapokuwa wazee hukosa furaha kwa sababu wanapoteza kazi walizokuwa wanazitegemea. Wanawake wazee huwa na furaha kwa sababu, kwa mtazamo wao huwa wameweza kumiliki vitu bora kabisa ambavyo mtu anaweza kutamani, nyumba na wajukuu wachache.

Bahati nzuri kwa mwanaume ni kujipatia nafasi inayoheshimika katika jamii. Lakini kwa mwanamke bahati ni kuuteka moyo wa mwanaume na kubaki nao katika maisha yake yote.

Mwanaume mara zote hutaka kumbadilisha mwanamke wa chaguo lake ili afuate dini na utaifa wake.

Kwa mwanamke ni rahisi kubadilisha dini yake na uraia kwa ajili ya mwanaume aliyempenda ikiwa ni pamoja na kubadilisha ubini wake baada ya kuolewa
 

Similar threads

Tofauti ya funzo tunalopata shuleni na lile tunalopata katika maisha; Kwanza kabisa nikusalimu wewe mpendwa wa kf ni muda sasa tangu tumeonana(kupitia madandiko), nikushukuru pia in advance kwa kunisamehe kwa mwandiko wangu, bado nadhidi kuimarika, moja kwa zote kwenye madaaa Katika maisha...
Replies
12
Views
392
Mimi somo la ujasiriamli sio mzuri ila leo tujadili kuhusu hivi vitu viwili Ujasiriamali na Biashara Ujasiriamali ni nini? Biashara ni nini? Vinatofautiamaje? Utajuaje huyu ni mjasiriamli na yule ni mfanyabiashara Kipi bora zaidi Kipi kinafaida kwa wengi? Stay tuned i will be back soon.
Replies
6
Views
332
Wakubwa shkamooni! Kiujumla inadaiwa wanawake ndio wana uo uwezo wa kutunza hela kuliko wanaume.. kwaili nakataa labda kama wanazungumzia wanawake wa zamani... Hawa wa siku hizi wanaspend sana kuliko men, wananunua kila kitu kilicho mbele yao, sijui ni ugonjwa? Kwa sisi men tuko vizuri mno...
Replies
33
Views
713
Licha ya kwamba aina zaidi za tofali za kujengea nyumba lakini watu wengi hujiuliza sana kati ya tofali za kuchoma na tofali za bloku au tofali za simenti ni zipi bora zaidi? angalau zipi zinafaa zaidi kwa ujenzi? kuhusu kulinganisha gharama za hizi aina mbili.
Replies
14
Views
604
Back
Top