- Joined
- Jul 3, 2023
- Messages
- 1,897
- Reaction score
- 3,986
- Points
- 113
Wakuu kwema!
Nimewamiss, sasa leo nimekuja na hii story ya jamaangu mmoja yeye ni fundi tv.
Huyu mwamba ni mtu safi ila tamaa ndio imemzidi, alikua anafanyakazi na mwenzake ofisi moja ila baadae wakashindwana kwahiyo kila mtu ikabidi awe na ofisi yake.. Yeye alipata bahati ya kukaa kwenye ofisi ya mwanzo iliyo zoeleka na watu.
Yule jamaa yake anaitwa Devi yeye akapata chumba kwa nyuma ya huyu mwamba yani hakuna umbali..
Sasa kwakua wateja baadhi walikua wamemzoea Devi wakawa wanakuja kumuulizia, jamaa akawa anawaambia hayupogo kabisa, na mara nyingine akajidai yeye ndiye Davi kwahyo akawa anapata riziki kupitia jina la Devi.
Sasa siku moja walikuja wateja na gari walikua watatu, wakaja ofisini kwa mkuu wakaulizia kwa Devi ni wapi? Jamaa akajibu hapa ndio kwa Devi, akaulizwa swali lingine Devi yuko wapi? Akasema mimi ndio Devi!
Kumbe Devi alifanya msala akakimbia wale ni polisi wanamtafuta... Jamaa wakajitambukisha wao ni polisi na wakamuweka mkuu chini ya ulinzi na akapelekwa moja kwa moja kituo cha polisi..
Alipofika kule kituoni ndio ikabidi awaeleze vizuri kuwa yeye sio Devi ila alijifanya ni yeye ili kama niwateja wampe kazi..
Sitori itaendelea
Ndugu zangu nazani mmepata cha kujifunza hapa, tujiamini sisi kama sisi sio lazima kuiba uhusika wa mtu, tujenge brandi(majina) zetu wenyewe ili tuje kufaidika nazo, hako ni chako, ridhiki ya mtu usiilalie mlango wazi...
Ukingangania vitu vizuri vya mtu kwa nguvu sio poa maana hata vitu vyake vibaya vinaweza kukungangania na wewe...
Ridhiki anaetoa ni Mungu, mbarikiwe sana